DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG - HANDENI, TANGA. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa. Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard ak...