Posts

TAGCO WAIKUMBUKA SHULE YA FAMILIA YA MZEE LAIBON ILIYOPO MTO WA MBU MKOANI MANYARA.

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Laiboni iliyopo Mto wa Mbu mkoani Manyara ,Rashid Mohamed msaada wa Madaftari 2500 kwa ajili ya wananfunzi wanaosoma katika shule hiyo. Mwenyekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas wakigawa Daftari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon. Mwenyekiti TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya kukabidhi Msaada huo. Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusuano Serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Laibon ,Rashid Mohamed wakati akikabidhi msaaada wa Matenki mawili ya kuhifadhia maji shuleni hapo .kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo. Mwenekiti wa TAGCO ,Pascal Shelutete akizungumza jambo na Wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Loibon. Moja ...

KAMPUNI YA KILIMANJARO SAR LTD YAINGIA MAKUBALIANO NA HOSPTALI YA ST JOSEPH YA KUTOA HUDUMA KWA WATALII WALIPATA MATATIZO MLIMA KILIMANJARO

Image
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun akitia saini makubaliano ya Mashirikiano na Hospitali ya St Joseph ya mjini Moshi kuhusu uanzishwaji wa Kliniki ya utoaji matibabu kwa Wagonjwa wanaopata matatizo wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro na Meru,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo huku zoezi hilo likishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (aliyesimama kulia) ,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya Kilimanjaro SAR,Amour Abdallah. Zoezi hilo la utiaji saini pia lilifanywa na Mganga Mfawidi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister Urbanie Lyimo kwa niaba ya Hospitali. Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kilimanjao SAR ,Ivan Braun na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya St Joseph ,Sister ,Urbanie Lyimo wakibadilishana karatasi zenye makubaliano ya kushirikiana katika utoaji wa matibabu kwa Wagonjwa waliopata matatizo kutokana na hali ya muinu...

UN waingia makubaliano na serikali kutangaza mpango wa maendeleo

Image
 Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akiwasilisha mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha. Ofisa Habari wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru akiuliza namna ambavyo mapambano dhidi ya rushwa yanavyoweza kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Suzan Mlawi (kulia) wakifuatilia mada kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia na uhusiano wake na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wakati wa mkutano wa 14 wa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea Jijini Arusha.  Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Maelezo Dk. Hassan Abbas akizungumza  na waandishi wa habari nje wakati wa mkuta...

DR. HASSAN ABASS AZINDUA TOVUTI YA MISA TANZANIA, JIJINI ARUSHA

Image
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto) wakizindua rasmi Tovuti ya MISA Tanzania inayopatikana hapa www.tanzania.misa.org  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas(wa kwanza Kulia) na  Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari(wa kwanza kushoto)pamoja na wadau mbalimbali ambao hawapo pichani wakipata maelezo kuhusiana na Tovuti ya MISA Tanzania kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva ambaye hayupo pichani. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw. Gasirigwa Sengiyumva(kulia) kulia akiendelea kutoa maelezo mbali mbali na vitu ambavyo vinapatikana katika Tovuti ya MISA Tanzania   Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Tovuti ya MISA Tanzania Jijini Arusha. TOVUTI INAPATIKANA HAPA www.tanzania.misa.org

WAZIRI WA HABARI ,SANAA,UTAMADUNI NA MICHEZO ,DKT HARSON MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI ARUSHA

Image
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamduni na Michezo Dkt Harson Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaofanyika kwa siku tano jijini Arusha. Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Sanaa,Utamaduni na Michezo ,Susan Mlawi akizungumza wakati wa mkutano huo. Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ,Dkt Hassan Abbas akizungumza katika mkutano hu unaofanyika katika Ukumbi wa mikuano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha. Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa 14 wa Chama cha maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kinachotajwa kama Kikao kazi wakifuatilia kwa karibu Hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa Ufunguzi wa mkutano huo. Mwenyekiti wa Chama cha...