Tizama:AJALI MBAYA WILAYANI HAI,40 WANUSURIKA KUFA ,KUPISHA MSAFARA WA JK .

Basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Tanga likiwa limepinduka jirani na njia panda ya uwanja wa ndege wa KIA.
Baadhi ya wasamalia wema wakitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali ya basi la Urio iliyotokea wilayani Hai jana.
Mmoja wa majeruhi akiwa amelala baada ya kupata mshtuko kufuatia ajali.
Basi linavyoonekana baada ya kupinduka.



Hai.

ZAIDI ya abiria 40 waliokuwa katika basi la Urio linalofanya safari zake kati ya mikoa ya Arusha na Lushoto-Tanga wamejeruhiwa vibaya baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kukwepa basi jingine katika makutano ya barabara ya kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio walisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha wakati magari hayo yakijiandaa kuanza safari mara baada ya kuzuiliwa kwa muda kupisha msafara wa Rais Kikwete.

Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni muda mchache msafara wa raisi Jakaya Kikwete kupita katika eneo hilo ukielekea uwanaja wa ndege wa KIA , ukitokea wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ambako Amefanya ziara ya siku mbili.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema baada ya msafara wa rais kupita magari yaliyokuwa yamesimamishwa kwa muda mrefu yaliondoka bila ya kuwa na mpangilio maalum hali iliyosababisha kutokee kwa ajali hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz hakuweza kupataikana mara moja kuzungumzia ajali hiyo kutokana na ugeni wa rais huku simu yake ikiita mara kadhaa bila ya kupokelewa .

 Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAZINDUA KITUO CHA KUTOA MSAADA WA KISHERIA