WAFANYAKAZI WA MABENKI MKOANI KILIMANJARO WALIVYOTOANA JASHO KATIKA BONANZA LA BANKERS DAY 2014,
Mashindano ya Mbio yalianza kwa upande wa wafanyakazi wa Benki tofauti tofauti wa Kiume. |
Wakimbiaji kwa upande wa kina mama nao walifanya maandalizi na hapa wakiongozwa na Meneja wa Azania Bank ,Hajira Mmambe9mweye kofia nyekundu) |
Waratibu wa Bonanza hilo wakijadiliana jambo kabla ya kufanyika kwa mbio za kina mama. |
Mbio za kwa kina mama zikaaanza na kumalizika mshindi wa kwanza na a Mwisho wote wakafahamika. |
Wafanyakazi wa Azania Bank wakiwa katika maandalizi ya mchezo wa kusukuma Gogo na hapa wanaongozwa na Meneja wao Hajira Mmambe. |
Wafanyakazi wa Uchumi Bank wakiwa katika maandalizi ya mchezo wa kusukuma Gogo . |
Benki ya KCB pia walikuwepo kuwakilisha katika mchezo huo. |
Kipyenga kikapulizwa shughuli ya kusukuma gogo ikaanza na mshindi akapatikana katika mzunguko wa kwanza Azania Bank wakawa wametakata . |
Mzunguko wa Pili wakakutana na wazee wa DTB Bank. |
Azania Bank Chali . |
Upande wa kufukuza Kuku wazee wa Bacrays Bank nao wakatakata. |
Kina mama nao wakamkimbiza Jogoo. |
Jogoo akakimbilia chini ya moja ya magarai yaliyokuwepo uwanjani hapo.shughuli ya kumkamata ikaendelea hadi uvunguni mwa gari. |
Hatimaye Jogoo akapatikana na mshindi pia akapatikana. |
Mwingine yeye aliambulia Manyoya ya mkiani. |
Kwenye mbio za Magunia pia wanaume wakaoneshana kazi . |
Kina mama nao wakaruka na maguni hadi mshindi akapataikana. |
Kazi ilikuwa ni hapa kwenye kuvuta kamba . |
Kamba ilikatika zaidi ya mara tatu hali iliyopelekea kushindwa kupatikana kwa mshindi hadi pale walipopunguza idadi ya watu. |
Wanaume wakaendelea kuvutana. |
Kina mama nao wakavutana . |
Kwa upande mpira wa Miguu kikosi cha CRDB Bank kilikuwa imara . |
Kikosi kingine kilikuwa ni hiki cha mchanganyiko wa Mabenki wakiwemo wale wa VICOBA. |
Mbungi la kufa mtu likapigwa. |
Wengine maji mwilini yalikata wakaamua kuongeza. |
Hoyaa na mimi niletee moja. |
Jamaa akagida migido kadhaa hapa kabla ya kurudi uwanjani. |
Wengine walipatiwa huduma ya kwanza. |
Meneja Masoko wa Kampuni ya Megatrade Investment ,Edmund Rutaraka pia alipata nafasi ya kuzungumza neno kama wadhamini wa Bonanza hilo. |
Mameneja wa matawi ya Benki zote zilizo shiriki Bonanza hilo wakiwa katika picha ya Pamoja. |
Wengine walishindana kucheza dance. |
Wengine walishiriki mchezo wa kukaa kwenye kiti. |
Zawadi zikatolewa kwa washindi pamoja na vyeti kwa kampuni zilizodhamini Bonanza hilo na benki. |
Comments
Post a Comment