Tizama:NYATI ALIVYOPAMBANA NA SIMBA 11 KATIKA HIFADHI YA SERENGETI .

Kundi la Simba likielekea katika mawindo yake baada ya kuona kundio la Nyati. Tukio hili lilijiri hivi karibuni katika Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania.
Simba wakianza kujipanga kwaajili ya mashambulizi katika kundi la Nyati 6 walio waona.
Nyati huyu ndio aliingia katika mtego na kuanza kufukuzwa na Simba. Kwa Mbali gari la Watalii likija eneo hilo na baada ya muda magari 12 yaliyo na watalii mbalimbali yalifika katika eneo hilo na kushuhudia mtanange mkali kati ya Simba na Nyati. Mpigapicha wa Gazeti la Uengereza la Daily Mail, Scott Macleod alinasa taswura hizi.
Simba wakianza jitihada za kumuangusha Nyati huyo dume bila mafanikio.
Ilikuwa ni vita ambayo haikuruhusu mtoto kutumwa maji dukani.
Ubabe wa Simba ilizidi kuongezeka kwa wafalme hao wa Pori kujaribu kumuua mmoja wa wanyama wakubwa 5 Porini. The Big 5 Animal
Watalii walikata kiu yao vya kutosha maana moja ya vitu vinavyowavutia watalii ni kumuona Simba au Chui akiwa mawandoni. Lakini hakika kwa Hifadhi za Tanzania hili linawezekana na watalii karibuni mjionee haya.
Mziki uliendelea ...
Watalii waliongezeka...jitihada za Simba walau kumuangusha Nyati hiyo biola mafanikio.
Simba hawakuhofua macho wala mingurumo ya magari iliyokuwa imewazunguka mahali hapo wakati vita yao ya kumla Nyati ikiendelea. Watalii wakifurahia kivutio hicho ndani ya ardhi ya Tanzania.
Hakika Nyati ni The Big 5 Animal. Licha ya Simba kuwa wengi lakini walishindwa kumuangusha Nyati huyu na kujipatia kitoweo. Simba walitawanyika kwenda kutafuta nguvu zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/