Posts

Showing posts from October, 2014

Breaking News:MTANGAZAJI WA ZAMANI WA RTD,BENKIKO AMEFARIKI DUNIA.

Image
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kiko enzi za uhai wake akiwa katika moja ya semina. MTANGAZAJI na mwandishi wa habari mkongwe nchini Ben Kiko amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Mhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. Ben Kiko ambaye jina lake kamili ni Ben Hamisi Kikoromo alihamishiwa katika hosptali ya Mhimbili kutokea hosptali ya Jeshi ya Milambo ya mkoani Tabora ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu kwa muda wa wiki mbili. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA, AMEEN Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania (RTD) sasa TBC,Ben Hamis Kikoromo maarufu kama Ben Kikoakizungumza na Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini Dixon Busagaga alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Cheyo mkoani Tabora wakati wa uhai wake.

WANAHABARI KILIMANJARO WATEMBELEA MUWSA.

Image
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira(MUWSA),Florah Stanley akifanya utambulisho kwa waandishi wa habari walipotembelea Mamlaka hiyo. Baadhi ya Wanahabari waliotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira(MUWSA) Meneja Fedha wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Moshi(MUWSA) Joyce Msiru akijitambulisha kwa wanahabari. Mwenyekiti wa TUICO tawi la MUWSA,Maulid Barie,Katibu wa TUICO tawi la MUWSA ,Jacob Olotu wakati wa ziara ya Waaandishi wa habari katika ofisi za Mamlaka hiyo. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wanahabari (hawako pichani)walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo. Toka shoto ni Meneja Biashara wa MUWSA,John Ndetiko ,Meneja rasilimali watu ,Michael Konyaki wakati wa kiako na wanahabari kilicho fanyika katika ukumbi wa Bodi ya MUWSA. Baadhi ya watendaji wa MUWSA. Meneja Ufundi wa MUWSA ,Patrick Kibasa akizungumza jambo wakati wa kikao hicho. M

JENGO LA NSSF KUBADILI TASWIRA YA MJI WA MOSHI.

Image
Jengo jipya linalojengwa na Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii  (NSSF) kukamilika kwake kutabadili taswira ya mji wa Moshi kwa kiasi kikubwa.Ni jengo ambalo limejengwa kisasa  ambalo kukamilika kwake kutapendezesha mji wa Moshi. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

WAZIRI NYALANDU ARUHUSU WANANCHI WANOENDA KWENYE MATIBABU KITUO CHA AFRICA AMINI KUPITA BILA KULIPA HIFADHINI.

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiwasili katika kituo cha Afya cha Africa Amini Alama kilichopo katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA)akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar. Waziri Nyalandu akisalimiana na wagonjwa waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kupata matibabu,Pembeni yake ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar. Mmoja wa wauguzi katika kituo hicho aliyefahamika kwa jina moja la Nice akitoa maelezo kwa Waziri Nyalandu,wengine ni Mbunge wa Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) Pascal Shelutete.  Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja wa wagonjwa aliyekuwa katika kituo hicho ambaye alihitaji kiasi cha shilingi 5000 kwa ajili ya matibabu pesa ambazo alisaidiwa na Waziri Nyalandu . Waziri Nyalandu akizungumza na mmoja ya watu waliofika katika kituo hicho kwa ajili  ya matibabu waliyefahamiana . Waziri Nyalandu akisamia wagonjwa.

WIZARA YA MALIASILI YABARIKI KUANZISHWA KWA MFUKO WA KULINDA MLIMA KILIMANJARO NA MLIMA MERU

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza wakati wa kikao kilicho shirikisha Kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Wabunge katika majimbo ya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Wakuu wa wilaya zinazopakana na mlima Kilimanjaro na mlima Meru,TANAPA na Idara ya Misitu,(kulia)ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Ibrahim Msengi. Naibu waziri wa TAMISEMI ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Siha ,akichangia wakati wa kikao cha kuanzishwa kwa mchakato wa uanzishwaji mfuko wa mlima Kilimanjaro na Mlima Meru ambao utalinda milima yote miwili. Makamau mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,Abdulkarim Shah akizungumza katika kikao hicho kimetokana na wabunge wa mkoa wa Kilimanjaro kuomba kuanzishwa kwa mfuko wa kulinda mlima Kilimanjaro. Baadhi ya washiriki wa kikao hicho kilichofanyika katika Hotel ya Sal salnero wakifuatilia michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho. Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,Agustino Mrema akichan