Posts

Showing posts from March, 2015

IGP ERNEST MANGU APANGUA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA YUMO gEOFREY KAMWELA WA KILIMANJARO.

Image
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi  ya makamanda wa polisi wa mikoa. Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.  Aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao makuu. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala  Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya. Wengine ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidi

MKUU WA WILAYA KINONDONI PAUL MAKONDA AKUTANA NA WANA UMOJA WA MAFUNDI MAGARI TEGETA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI DHIDI YA MWEKEZAJI

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na Viongozi wa Umoja wa Mafundi Magari Tegeta wakati akikagua eneo lenye mgogoro wa ardhi kati ya wanaumoja huo pamoja na mwekezaji alipokwenda kuwasikiliza kuhusu mgogoro huo Dar es Salaam jana. DC Paul Makonda akiwahutubia wana umoja huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akiwa na viongozi wa umoja huo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Nationi Ndela akitoa historia ya mgogoro huo mbele ya DC Makonda. Baadhi ya mafundi magari katika gereji za Tegeta wakimsikiliza DC Makonda wakati akiwahutubia ili kupata muafaka wa mgogoro huo Baadhi ya gereji zilizopo katika eneo hilo la mgogoro. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (katikati), akijaribu moja ya mashine ya kuchonga vyuma iliyopo katika eneo hilo. Baadhi ya mafundi na wamiliki wa gereji mbalimbali katika eneo hilo la mgogoro wakimsikiliza DC Makonda. Wanaumoja hao wakiwa kwenye mkutano huo Hapa DC Paul Makonda akizung

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI KIGOMA WAZINDUA GAZETI LAO LA KIGOMA YETU

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini Exavery Maketa akisoma hotuba yake kwa wageni waalikwa (Hawapo pichani)kwa niaba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma(KGPC) Deogratius Nsokolo akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa walihudhuria uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU. Baadhi ya viongozi wa serekali na dini waliohudhulia katika uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU Waandishi wa gazeti la Kigoma YETU wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa gazeti hilo  Waandishi wa chama cha habari mkoa wa Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Exavery Maketa baada ya uzinduzi wa gazeti la Kigoma YETU Wandishi wa Gazeti la kigoma yetu wakifurahia baada ya uzinduzi kutoka kushoto ni Mwajabu Kigaza wakatikati ni Rhoda Ezekiel pamoja na Editha Karlo.  Na Editha Karlo wa  Globu ya Jamii, Kigoma  KWA niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Ma

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA WILAYA YA ROMBO

Image
Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakirejesha kadi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara  Wakazi wa Tarakea wakifurahia jambo wakati katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihutubia Pichani kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi na Katibu wa Mbunge wa CHADEMA,wilaya ya Rombo John Tarimo akitangaza rasmi kurejea chama cha CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza Mmoja wa Wakazi wa Rombo akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwa furaha kubwa kama aonekanavyo pichani    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vikundi vya utamaduni wakati akiwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Rombo. Baadhi ya Vijana kwa niaba ya vijana zaidi ya 900 wa Boda boda wakiwa wamekabidhiwa  vyeti vya Bima ya Afya ya jamii. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akiwahutubia wananchi wa Rombo kabla ya kufungua ofisi ya CCM wilaya ya Rombo ambapo aliwaambia wananchi hao

WANACHAMA WA TUICO TAWI LA MUWSA ,WAPATA VIONGOZI WAPYA.

Image
Baadhi ya wanachama wakijiandaa kwa ajili ya kuchagua viongozi wa TUICO,tawi la MUWSA. Mwenyekiti wa TUICO mkoa wa Kilimanjaro,Renatus Chimola akikusanya kura kwa nafasi ya Uenyekiti. Wanachama wakisikiliza sera toka kwa wagombea. Baadhi ya wanachama wakijinadi mbele ya wanachama wa TUICO tawi la MUWSA ,kuomba ridhaa ya kuingoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa kamati ya utendaji ya TUICO tawi la MUWSA ,Esther Massawe akiomba kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo. Kamati ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUICO tawi la MWSA wakiendelea na zoezi la kuhesabu kura. Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa Viongozi wa TUICO,tawi la MUWSA ,Rashid Nachan akitangaza matokeo . Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira MUWSA ambao ni wanachama wa TUICO wakifurahia mara baada ya kutangazwa kwa washindi. Mwenyekiti wa TUICO mkoa wa Kilimanjaro,Renatus Chimola akizungumza mara baad