MADAKTARI WA DIASPORA WAKABIDHI MSAADA WA DAWA ZA MAGONJWA YA BINADAMU KWA HOSPTALI YA MNAZI MMOJA

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr. Jidawi akizungumza na Madaktari Diaspora kutoka Washington walipofika Afisini kwake kwa kujutambulisha ujio wao Zanzibar walioletwa na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiwa chini ya uenyeji wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),wakiwa Zanzibar wametoa huduma ya kucheki waginjwa wa Kisukari na Meno na kutoa Elimu ya Afya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar.   
Katibu Mkuu Dr Jidawi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Madaktari hao walipofika Afisini kwake wakiwa na Ujumbe wa Watu 17 wakiwemo Madaktari wa Saratani ya Matiti kwa Kina mama, Kisukari na Meno.
Madktari wa Diaspora kutoka Washington wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar walipofika Afisi kwake 
Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai wakiwa na wenyeji wao wakifuatilia maongezi na Dr Jidawi walipofika kuwatambulisha madaktari hao. kupitia Jumuiya ya Watanzania Washington
Mkuu wa Ujumbe huo,Rais wa Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Mkuu wa Ujumbe huo Rais wa Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Daktari wa Meno akuzungumza wakati wa mkutano huo na Katibu Mkuu Wizaya ya Afya Zanzibar walipofika Afisini kwake kujitambulisha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Saleh Mohammed Jidawi akipokea msaada wa Dawa za Binaadamu kutoka kwa Daktari  Jummy Amuwo kwa niaba ya Madaktari wa Dispora kutoka Washington  wakiwa Zanzibar  mualiko wa Jumuiya ya Watanzania Washingto, akishuhudia Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid, makabidhiano hayo yamefanyika katika Afisi za Wizara ya Afya Zanzibar
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washington Ndg Iddi akiungezani na Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid baada ya makabidhiano ya madawa ya Binaadamu yaliotolewa na Madaktari Diaspora Washington. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya Zanzibar. 
 Wakipongezani kwa ushirikiano waliouonesha kwa mapokezi waliopata wakipongezana baada ya hafla hiyo.


Wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Wizara ya Afya Zanzibar, baada ya hafla ya kukubidhi msaada wa dawa
Madaktari Diaspora wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar nje ya Jengo Wizara ya Afya Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi dawa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Jidawi.
Picha zote na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.Com. 

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/