TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK
Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania. Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza kutumia Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada. Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za kampuni. Hivi karibuni, Tigo Tanzania imejishindia tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambayo inatambua mashirikana watu bina