Posts

Showing posts from April, 2016

MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO.

Image
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema)  mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.  Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava . Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko. Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko. Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Hivi ndivyo hali inavyoonekana. Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini

MWANAHABARI MTOTO NA MWANAMAZINGIRA WA UN, GETRUDE CLEMENT AWASILI JIJINI MWANZA.

Image
Shujaa Wetu, Mwanahabari Mtoto, Mwanamazingira Balozi wa Umoja wa Mataifa UN kutoka Mwanza Tz, Getrude Clement (16) jana amewasili nyumbani Jijini Mwanza majira ya saa tatu usiku na kupokelewa kwa shangwe na ndugu, jamaa na marafiki katika Uwanja wa Ndege Mwanza. Alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani uliohusu Mabadiliko ya Tabia nchi (Climate Change) ambapo alihutubia õakiwakilisha kundi la Watoto na Vijana duniani. Kutoka Kushoto Pichani ni Brightius Titus ambae ni Katibu wa Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza MYCN, Katikati ni Getrude mmoja wa Watoto wa Mtandao huo na Kulia ni Shaban Magana ambae ni Mwenyekiti wa MYCN.

WANANCHI WA ITOBO, ITIRIMA - SIMIYU WAASWA KUZAA KWA KUFUATA UZAZI WA MPANGO

Image
Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Picha/Video na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango. Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima.  --- Na Cathbert Kajuna - Itirima, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wameaswa kuachana na mila za kuzaa watoto wasio kuwa na idadi ili kuepusha taifa lenye wategemezi wengi. Akizungumza katika mafunzo ya Uzazi wa Mpango yaliyotolewa wiki iliyopita na Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena alisema kuwa kuna

DC NOVATUS MAKUNGA AJIONEA ATHARI ZA MAFURIKO KATIKA WILAYA YA MOSHI

Image
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko. Mkuu wa wilaya akiwa katika uwanja wa ndege wa Moshi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda kujionea hali ya mafuriko katika maeneo mbalimbali. Mtaalamau anayeshughulikia Majanga kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Canon Masanja (wa tatu toka kulia) akimuelekeza jambo rubani muda mfupi kabla ya ndege kuruka. Mkuu wa wilaya ya Moshi akiteta jambo na Kaimu meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro muda mfupi kabla ya kwenda kutizama eneo lililo athirika kwa mafuriko. Maeneo mbalimbali ,zikiwemo nyumba zikiwa zimezingirwa na maji katika vijiji vya Miwaleni huku mashamba yakiwa yameharbika vibaya. Mioundo mbinu ya barabara pia imeathirika vibaya. Maashamba yamejaa maji , Maeneo mengine ba

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO SAID MECKY SADICK AFANYA KIKAO NA WATUMISHI WILAYA YA HAI.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na watumishi,wakuu wa idara za Halmashauri na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika wilaya ya Hai wakati wa kikao cha utamburisho kilichoafnyika katika ukumbi wa KKKT Bomang'ombe. Baadhi ya viongozi wa Taasisi mbalimbali katika wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho. Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho. Baadhi ya watumishi na viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika kikao hicho. Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Hai,Said Mderu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa katika kikao hicho. Baadhi ya Wenyeviti wa vitobgoji na vijiji, Baadhi ya Wenyeviti wa vitongoji na vijiji wakiuliza maswali wakati wa kikao hicho. Viongozi wa dini pia waliwasilisha hoja zao kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini