MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO.
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .
Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.
Sehemu ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.
Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Hivi ndivyo hali inavyoonekana.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya.
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa.
.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB) Jaffer Machano akizungumza wakati wa kikao kifupi kati ya uongozi wa TIB na ule wa Manispaa ya Moshi juu ya Ujenzi wa kituo kipya cha kisasa cha Mabasi cha Ngangamfumuni . Kikao kinaendelea. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Jafary Michael akizungumza wakati wa kikao hicho. Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ,Shaban Ntarambe akitoa neno la shukrani wakati ujumbe wa Benki ya Rasilimanli nchini TIB ulipotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kukabidhi michoro halisi ya kituo kikuu cha mabasi cha kisasa cha Ngangamfumuni . Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB) Peter Noni akimkabidhi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary Michael ,CD ya mchoro halisi wa Jengo la kisasa la kituo kikuu cha Mabasi cha Ngangamfumuni mkoani Kilimanjaro Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB) Peter Noni akimkabidhi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Jafary Michael...
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof Lughano Kusiluka akisisitiza jambo kwa wanafunzi chuo hicho kitivo cha Sheria alipowataka kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha Sheria chuoni hapo Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kituo cha Msaada wa kisheria katika Chuo Kikuu cha akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanzishwa kwa kituo cha msaada wa kisheria chuo kikuu Mzumbe Mkoani Morogoro anayefata alieshikilia vitabu ni makamu mkuu wa chuo kikuu cha mzumbe Prof, Lughano Kusiluka
Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Moshi vijijini ,Hussein Jamal akizungumza wakati wa kikao cha makatibu kata na makatibu wa matawi kilichofanyika katika hotel ya King Size Himo. Mwenyekiti wa Makatibu katika jimbo la Vunjo ,Shaban Mwangi akisoma taarifa ambayo inadaiwa kupikwa kwa lengo la kukivuruga chama hicho katika jimbo la Vunjo. Baadhi ya viongozi wakisilikiliza kwa makini. Naibu kamanda wa vijana wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Shirima akizungumza wakati wa kikao hicho kilichokuwa na lengo la kurudisha hali ya amani na umoja ndani ya chama cha mapinduzi jimbo la Vunjo. Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi vijijini Miriam Kaaya akizungumza wakati wa kikao hicho ambacho kilijadili pia tuhuma zilizotolewa dhidi yake. Makatibu wakila kiapo . Baadhi ya makatibu katika kikao hicho. Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Comments
Post a Comment