Posts

Showing posts from June, 2016

AZANIA BANK TAWI LA MOSHI YAFUTURISHA WATEJA WAKE.

Image
Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi Hajira Mmambe akiwakaribisha wageni kupatra futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wake. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick na Mkuu mpya wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba pia walikua ni miongoni mwa wageni waalikwa. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza wakati wa Futuru iliyoandaliwa na Benki ya Azania tawi la Moshi . \Baadhi ya wageni wakifuatilia hotuba iliyoyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick (hayupo pichani) wakati wa Futuru iliyoandaliwa na Benki ya Azania tawi la Moshi. Meneja wa Azania Benk tawi la Moshi ,Hajira Mmambe akiwakaribisha wageni katika Futuru iliyoandaliwa kwa wateja wa benki hiyo,hafla fupi iliyofanykika katika uwanja wa gofu wa Moshi maarufu kama Moshii Club. Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadick walijumuika katika hafla hiyo. Baadhi ya wageni waalikwa wakipata Futari. Mkuu mp

TANAPA YASAIDIA UJENZI WA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YANAYOPAKANA NA HIFADHI YA TAIFA MILIMA YA MAHALE ILIYOPO MKOANI KIGOMA.

Image
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale,Mhifadhi Romanus Mkonda akizungumza juu ya ujenzi wa madaraja ulioanza katika barabara ya kuelekea katika hifadhi hiyo. Wanahabari wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza ,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA). Kibao kinachoonesha taarifa mbalimbali juu ya ujenzi wa daraja hilo. Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa. Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi. Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya usafiri na hata mifugo imekua ikipi

WANAHABARI WATEMBELEA VIJIJI VINAVYO PAKANA NA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE.

Image
Baadhi ya Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inayosifika kwa uwepo wa Sokwe Mtu. Usafiri unaotegemewa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ni Boti na Mitumbwi . Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,Pascal Shelutete (Mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda wakielekea katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi hiyo,Wengine ni wmwandishi wa gazeti la Uhuru,Jackline Massano na kulia ni Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Mkinga Mkinga. Wanahabari ,Said Mnekano maarufu kama Bonge wa Clouds fm,aliyesimama nyuma.akiwa na Asiraji Mvungi pamoja na muongoza watalii ,Rashid Omary wakiwa katika moja ya boti zinazotumika kama njia ya usafiri katika Hifadhi ya  Taifa ya Mahale. Waandishi ,Beatrice Shayo na Nora Damian wakijaribu kushuka kutoka katika boti. Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Sh

TANAPA YATOA ZAIDI YA MILIONI 600 KUSAIDIA VIKUNDI 70 VILIVYOKO MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA VINAVYOZUNGUKA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE

Image
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Romanus Mkonda akitoa maelezo mafupi mbele tya waandishi wa habari waliotembelea vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo iliyopo mkoani Kigoma. Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda akizungumza na wananchama wa vikundi vya kijasiliamali vinavyojulikana kama COCOBA vinavyosaidiwa na hifadhi hiyo (hawapo pichani. Baadhi ya wanachama wa vikundi wakiwa katika mkutano na watumishi wa TANAPA pamoja na wanahabari waliotembelea vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale . Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza katika mkutano huo ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda. Baadhi ya Wanahabari walioitembelea vijiji hivyo. Mwenyekiti wa kijiji cha Katumbi ,Issa Zuber ,kijiji kimojawapo ambacho wanachi wananufaika