TANAPA YATOA ZAIDI YA MILIONI 600 KUSAIDIA VIKUNDI 70 VILIVYOKO MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA VINAVYOZUNGUKA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Romanus Mkonda akitoa maelezo mafupi mbele tya waandishi wa habari waliotembelea vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo iliyopo mkoani Kigoma.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda akizungumza na wananchama wa vikundi vya kijasiliamali vinavyojulikana kama COCOBA vinavyosaidiwa na hifadhi hiyo (hawapo pichani.
Baadhi ya wanachama wa vikundi wakiwa katika mkutano na watumishi wa TANAPA pamoja na wanahabari waliotembelea vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza katika mkutano huo ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda.
Baadhi ya Wanahabari walioitembelea vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Katumbi ,Issa Zuber ,kijiji kimojawapo ambacho wanachi wananufaika na msaada wa mafunzo ya ujasiliamali unaotolewa na TANAPA,
Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano ,Juma Makumbi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Pascal Shelutete mara baada ya kuzungumza na wanachama wa vikundi vinavyopewa msaada na shirika hilo .
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.
Wananchi
wa vijiji vya Buhungu
na Konkwa vilivyoko
mwambao mwa ziwa Tanganyika wilaya
Uvinza mkoani Kigoma
wanalazimika kuhifadhi mamilioni
ya fedha za
miradi ya vikundi
vyao kwenye masanduku
ya chuma na
kuyafukia chini ya
ardhi kutokana na
ukosefu wa huduma
za taasisi za fedha
utaratibu waliodai kuwa
unaotishia usalama wa
fedha hizo na
pia maisha yao .
Wananchi hao
pamoja na kuwashukuru
wadau wanaowasaidia likiwemo
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Hifadhi
yake ya Milima ya Mahale wamesema wanatumia njia
hiyo kutokana na
kuogopa kusafirisha kiasi
kikubwa cha fedha
umbali mrefu ili
kuzifikia taasisi za
fedha zilizoko kigoma
mjini na wameiomba serikali
na asasi za
fedha kusogeza huduma
katika maeneo ya vijijini.
Mkufunzi mkuu wa vikundi vya benki ya jamii ya
uhifadhi (COCOBA) vinavyo fadhiliwa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA),
Simada Andrea amesema kuwa vikundi hivyo
vinavyoizunguka hifadhi ya milima ya mahale, vina sifa za kupewa mikopo lakini
benki zimekuwa zikiwakataa na kuwapa masharti magumu.
“Sifa za kupewa mikopo wanazo…tatizo benki zinakataa
kuwakopesha kwa sababu ya umbali, zinawataka watu wa mijini kwa madai kuwa
wataweza kuwafuatilia,” alisema.
Alisema vikundi hivyo, vimesajiliwa na serikali za
vijiji na halmashauri ya wilaya ya uvinza iliwahi kuvikopesha kwa majaribio sh.
milioni 3 na vikarudisha kwa wakati.
“Naomba niziambie benki kuwa vikundi vya cocoba
vinakopesheka na vinalipa kwa wakati,” alisema.
Hata hivyo, Andrea aliziomba taasisi hizo za kifedha
kupeleka huduma katika maeneo yao ili ziwawezeshe kufanya shughuli zao kwa
urahisi na kwa uhuru hatua itakayowaongezea tija na ufanisi.
Naye, afisa mtendaji wa kijiji cha Nkonkwa, Issa Fungameza
alisema kuna vikundi hivyo kwa sasa vinatunza fedha zao katika kiboksi cha
chuma kutokana na benki kuwa mbali.
“Vikundi vinakopesheka, kwa kuwa benki ziko mbali
hivyo wanashindwa kupeleka fedha hizo benki na kuamua kuzitunza kwenye kiboksi
cha chuma,” alisema.
fungameza aliiomba serikali kuliangalia suala hilo
kwa undani zaidi kwa kuvikopessha vikundi hivyo ili viweze kujiinua kiuchumi na
kimaendeleo.
Mkuu wa idara ya ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya
Mahale,Romanus Mkonda alisema TANAPA imetoa
zaidi ya milioni
600 kuvisaidia vikundi
zaidi ya 70
vya wananchi katika
vijiji hivyo kupata
mafunzo ya ujasiria mali , uhifadhi
wa mazingira na
mitaji, hatua inayolenga
kuwaepusha wananchi hao
kujihusisha na uharibifu
wa mazingira na
ujangili katika maeneo
yaliyohifadhiwa ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale
Mwisho.
Comments
Post a Comment