MRADI WA URASIMISHAJI ARDHI UBUNGO WAINGIA MIZENGWE WATENDAJI WATISHIA KOGOMA KWA KUKOSA POSHO

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi



Na Dotto Mwaibale

WATENDAJI na vibarua wanaofanya kazi ya kupima ardhi katika mradi wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela katika Kata ya Kimara 
wilayani Ubungo umeingia mdudu baada ya kutishia kugoma kutokana na kutolipwa fedha za posho ya kazi hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu.

Hatua hiyo imefikiwa baana ya kuona baadhi ya vongozi wanaosimamia mradi huo wa kuanza kujinufaisha wenyewe na kuwanyonya watendaji wakiwemo vibarua 
hao.

Wafanyakazi wa upimaji wa ardhi kutoka wizarani na vibarua hao wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili kwa masharti ya kuto andikwa majina yao gazetini 
wamesema  viongozi hao kupitia mradi huo wamejenga mazingira ya  kujinufaisha kupitia fedha zilizotoka Benki ya Dunia kufanya mradi huo.

"Tunachangamoto kubwa ya kupata fedha za malipo kwa kazi tunayoifanya tumefanya kazi miezi minne lakini tumelipwa mwezi mmoja tu na si sisi peke yetu na hata 
watendaji wa wizara wanaofanya kazi hii nao hawajalipwa wakati fedha zipo " alisema mmoja wa vibarua hao.

Kibarua huyo alisema kuwa kuna mmoja wa kiongozi wa wizara hiyo anayesimamia mradi huo ndiye kikwazo kikubwa cha mradi huo na jitihada za makusudi 
zisipochukuliwa mradi huo hautafikia malengo yake.

“Binafsi acha niseme ukweli mradi huu ulianza vizuri lakini sasa utakwama kwani viongozi waliopo pale wizarani wameanza kutumia fedha vibaya na hawataki kutupa
licha ya fedha za mradi kuwepo na tunapowadai wanasema eti Rais John Magufuli hajaidhinisha fedha hizo wakati sio kweli" alisema mtendaji mwingine wa 
mradi huo kutoka wizarani.

Mtendaji huyo alisema changamoto hiyo yakutopewa fedha zao imewapunguzia mori wa kazi hivyo kuingia mashaka kama mradi huo utakwisha.


“Kiukweli ndugu mwandishi hapa watu wanaishi kama ndege wafanyakazi kila kukicha ila hawajalipwa mwezi wa tatu, ukiangalia kwa sasa wanasema eti hela zao 
zimetoka ila wanalipwa siku 20 wakati mwezi unasiku 30 sasa hizo hela zinazobaki za siku 10 viongozi wanazipeleka wapi? kama si wizi wa macho macho" alihoji 
mtendaji huyo.

Mtendaji huyo aliongeza kuwa jambo hilo limekuwa ni janga kwani watendaji wa mradi huo wapo zaidi ya 50 sasa anapokatwa siku 10 kila mmoja anapata 
shilingi ngapi hanazikosa na fedha hizo zinapelekwa wapi.

Akizungumzia changamoto hiyo Diwani wa Kata ya Kimara ambapo mradi huo upo, Pascal Manota alikiri kwa watendaji hao kutolipwa fedha hizo na tayari amekwisha 
mjulisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi juu ya changamoto hiyo.

"Changamoto kubwa ipo kwa viongozi wa wizara waliopewa kufanyakazi hiyo fedha zipo lakini hawawalipi watendaji hali inayozoofisha mradi huo tunamuomba 
waziri aliangalie suala hilo kwa karibu kabla ya mambo kuharibika" alisema Manota.

Manota alisema watendaji hao wa serikali hivi sasa wapo tu ofisini wakisoma magazeti hawana ari ya kazi hali hii imechangiwa na viongozi hao wasiokwenda na kasi ya Rais wetu Dk. John Magufuli ya hapa kazi tu.

Jitihada za gazeti hili za kumpata mratibu wa urasimishaji wa ardhi wa wizara hiyo ambaye anasimamia mradi huo, Lydia Bagenda zilishindikana baada ya kwenda 
ofisini kwake na kuambiwa alikuwa nje ya ofisi kikazi na hata halipopigiwa simu mara kadhaa simu yake ilikuwa imefungwa.






Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/