Posts

Showing posts from March, 2017

MTANZANIA ALIYEWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO AMUANGUKIA MWAKYEMBE.

Image
Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka. Gaudence Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka rekodi baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu. Lekule akifurahia mara baada ya kufanikiwa kuweka ekodi ya kutumia muda wa saa 8:36 kupanda Mlima Kilimajaro na kushuka. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. MTANZANIA ,Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa. Lekule anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda kwa muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36 alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi bi

MUWSA WATUMIA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KUOTESHA MITI KATIKA VYANZO VYAKE

Image
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishusha miti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya vyanz vya maji vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo. Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba mti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya chanzo cha maji cha Shiri kilichopo wilayani Hai. Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisaidia katika zoezi la ubebabji miti kwa ajili ya kuotesha. Wafanyakazi wa MUWSA wakiwa wamebeba mit kwa ajili ya kuotesha katika chanzo cha maji cha Shiri. Kaimu Mkurugenzi wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji cha Shiri. Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiotesha miti katika chanzo hicho. Hii ni sehemu ya mitiiliyooteshwa Mwaka jana katika eneo hilo zoezi lililooongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Saidi Mecky Sadicki. Huu ndio mti uliooteshwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanja

TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAKABIDHIWA BENDERA ,YAELEKEA UGANDA NA MATUMAINI YA KURUDI NA MEDALI.

Image
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akikabidhi Bendera kwa manahodha wa timu ya taifa ya riadha kwa upande wa wanaume,Fabian Joseph (kushoto) na Magdalena Shauri (kulia)Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru (mwenye miwani) ,Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na kushoto ni Meneja wa timu ya taifa ya riadha Meta Petro. Raisi wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akizungumza na wanariadha 28 wanaoelekea nchini Uganda kwa ajili ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru akitoa neno kwa wanariadha hao,Shirika la Hifadhi za Taifa ndilo limedhamini wanariadha hao ambao idadi yao katika ushiriki wa mbio hizo imevunja rekodi ya tangu mwaka 1991. Baadhi ya wanariadha watakao iwakilisha nchi katika mashindano hayo yat

DAWASCO KUTUMIA WIKI YA MAJI KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KUHUSU HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJI TAKA.

Image
                        Na Mwandishi wetu. Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limepanga kutumia maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji inayoanza kesho kutoa elimu ,kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya DAWASCO vilivyopo katika Jiji la Dar es salaam , Miji  ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani. Utaratibu huu umelenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka Dawasco ,kupata Elimu ya Huduma ya Maji   na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya DAWASCO na wananchi. Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Everlast Lyaro amesema madawati haya yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa wiki nzima ya maadhimisho haya ya wiki ya Maji. Amesema zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi litafanyika hadi siku za Jumamosi na Jumapili ambapo Madawati yatakuwa wazi ili kutoa nafasi zaidi kwa wananchi wen

JK AZINDUA RASMI TAASISI YA MAENDELEO YA JAKAYA MRISHO KIKWETE (JMKF)

Image
 Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine  itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani. Na. Immaculate Makilika- MAELEZO Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anapenda kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na jamii. Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa  akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete Foundation)  alisema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendel