DAWASCO KUTUMIA WIKI YA MAJI KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KUHUSU HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJI TAKA.
Shirika
la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limepanga kutumia
maadhimisho ya 29 ya wiki ya maji inayoanza kesho kutoa elimu ,kusikiliza kero
na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati maalumu katika vituo vyote 10 vya
DAWASCO vilivyopo katika Jiji la Dar es salaam , Miji ya Kibaha na Bagamoyo
mkoani Pwani.
Utaratibu
huu umelenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka Dawasco
,kupata Elimu ya Huduma ya Maji na
kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya DAWASCO na
wananchi.
Kaimu
Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) Everlast Lyaro amesema madawati haya yatakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa
wiki nzima ya maadhimisho haya ya wiki ya Maji.
Amesema
zoezi la kupokea kero na malalamiko kwa waanchi litafanyika hadi siku za
Jumamosi na Jumapili ambapo Madawati yatakuwa wazi ili kutoa nafasi zaidi kwa
wananchi wengi kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa utatuzi.
Uzinduzi
wa maadhimisho ya wiki ya maji utafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na
mgeni rasmi anatazamiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda
ambapo pamoja na mambo mengine Dawasco itapokea miradi ya Jumuiya za watumia maji
katika maeneo mbalimbali.
Maadhimisho
ya wiki ya Maji yameanza rasmi leo Machi 16 hadi Machi 22 mwaka huu yakibeba kauli
mbiu ya “MAJISAFI NA MAJITAKA- PUNGUZA
UCHAFUZI YATUMIKE KWA UFANISI”
Wakati
huo huo shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) linaendelea
na zoezi maalum la ubadilishaji wa Mita za Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es
salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.
Zoezi
hilo lililoanza mapema October 2016, linalenga kuondoa mita zote za Maji ambazo
ni chakavu, Mbovu na zenye muda mrefu
katika makazi ya watu, taasisi pamoja na viwanda ambalo linaenda sanjari na ufungaji wa Mita mpya za Maji kwenye maeneo
mbalimbali.
Kaimu
Meneja Uhusiano wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) Everlast Lyaro amesema tangu kuanza kwa zoezi hili tayari mita za
Maji takribani 25,000 zimekwisha badilishwa na kwamba uondoaji wa mita Chakavu una
lengo la kuongeza ufanisi katika usomaji wa Mita kwa usahihi, kupunguza kiasi
cha Maji kinachopotea kutokana na uchakavu na kuakisi matumizi halisi ya Maji
yanayotumiwa na mteja.
Mwisho.
Comments
Post a Comment