SIKU YA TATU YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU KATIKA MLIMA KILIMANJARO KWA WAZALENDO 47 KWA AJILI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU PAMOJA NA KUTANGAZA UTALII WA NDANI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,Jenerali,George Waitara akiwa katika maandalizi ya kuianza siku ya tatu ya Wazalendo 47 kuelekea katika kilele cha Uhuru ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru . Baada ya kupumzika kwa muda katikia kituo cha Horombo Wazalendo kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ,Waandishi wa Habari,Marafiki wa China na Tanzania pamoja na Watumishi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) walianza safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo kabla ya kuelekea kilele cha Uhuru. Safari ilianza kwa Slogan ile ile ya "Mdogo Mdogo" Baadae Safari ikaingia kwenye barabara yenye mawe hivyo utembeaji katika eneo hili ulihitaji uangalifu wa hali ya juu. Wengine walitengeneza Tabasamu kuonesha safari itamalizika kwa salama. Safari iliendelea na kila mmoja alipambana na hali yake. Hatimaye Wazalendo wakaiacha misitu mifupi bna kuingia katika kituo cha mwisho kabisa yanapotiririka maji. Hapa Wanapaita "Last Wot