Posts

Showing posts from November, 2024

BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI

Image
 BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI #KAZIINAONGEA  Katika kuendelea  kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.   Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi. Aidha Katika vitongoji 1849 vya  Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA

Image
 SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA #KAZIINAONGEA Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa Maji kwa  wananchi wake, hivyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo ni Mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia vijiji 9 na Mradi wa Nkinga Simbo utakaohudumia vijiji 8 vilivyopo jimbo la Manonga Mkoani Tabora. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali, aliyeuliza lini Serikali itatenga Fedha za ujenzi wa Miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale - Manonga. Mhandisi Kundo amesema Mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata za Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilisha miradi hiyo. Amesema  Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa vijiji vya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika kata ya Igoweko.

SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000

Image
 SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000 #KAZI INAONGEA Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetaka gharama ya kuweka umeme kwa vijiji vyote nchini iwe ji tsh.27,000 na sio zaidi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Jijini Dodoma hivi karibuni. Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, Kapinga alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili yaweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000. Akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme ya  zaidi ya 27,000. "Kuna baadhi ya maeneo ambayo ni Vijiji yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, , namuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kufanya mapitio ya maeneo haya