KONGAMANO LA UHURU WA HABARI WPFD KUFANYIKA MOROGORO MEI 2-3, WADAU ZAIDI YA 200 KUSHIRIKI
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani (WPFD) yatakayofanyika tarehe 2 mwezi Mei mwaka huu mkoani Morogoro. Na Modewjiblog team Wanahabari na wadau wa habari wanatarajiwa kukutana Mkoani Morogoro kwa siku mbili kwa kusanyiko la maadhimisho ya siku ya Uhuru wa habari duniani (WPFD), litakalofanyika katika hoteli ya Nasheera, Mjini Morogoro. Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), Ndugu Simon Berege alieleza kuwa, kusanyiko hilo la wandishi wa habari na wadau wa habari litafanyika mjini humo Mei 2-3, mwaka huu. “Hii ni mara ya kwanza WPFD kuadhimishwa mkoani Morogoro na mwakani itafanyika mkoa mwingine nia ni kufanya kila mkoa kupata nafasi ya kuadhimisha siku hiyo. Wakati...