Posts

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI KANDA YA KASKAZINI.

Image
Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini ulitanguliwa na maandamano yaliyopita katika barabara mbalimbali za mji wa Moshi na kuhitimishwa katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi. Washiriki kutoka Asasi mbalimbali wakipita mbele na mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini. Baadhi ya viongozi wa taasisi mablimbali wakiwa wameketi meza kuu na mgeni rasmi wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini Said Mecky Sadiki. Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,Elizabeth Mushi akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatli wa kijinsia. Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Elizabeth Mushi akipeana mkono na Mgeni rasmi katika unzinduzi huo,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki mara baada ya kutoa taarifa juu ya ukatili. Mkuu w...

WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA MSASA

Image
Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena akitoa mada.   Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena (kulia), akiwasilisha mada juu ya jinsi ya kuingiza masuala ya jinsia katika mpango kazi wa taasisi wakati wa kikao kazi cha watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilicho fanyika leo katika Ukumbi wa ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.   Mafunzo yakitolewa. Picha ya pamoja na mkufunzi. (Imeandaliwa na Monica Laurent wa Ofisi ya Msajili wa Vyama)

HAKUNA KIONGOZI WA JUU WA SERIKALI ANYEPINGA ZOEZI LA UHIFADHI NCHINI – MAJALIWA

Image
Na Hamza Temba - WMU Kufuatia malalamiko ya wahifadhi juu ya kauli na vitendo mbalimbali za baadhi ya wananchi na viongozi wa kisiasa vyenye lengo la kukwamisha shughuli za uhifadhi nchini kwa maslahi yao binafsi kwa visingizio kuwa ni maagizo kutoka juu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa tamko na kusema kuwa hakuna kiongozi wa juu wa Serikali anayepinga zoezi la uhifadhi wa maliasili nchini. Majaliwa ameyasema hayo juzi wakati akizungumza na viongozi na watendaji wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakuu wa taasisi za uhifadhi zilizopo chini ya wizara hiyo na wakuu wa hifadhi za taifa pamoja na mapori ya akiba katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma. “Wapo watu wanaotumia majina ya viongozi wakuu kukwamisha mazoezi yanayoendeshwa na wahifadhi nchini. Hakuna kiongozi wa juu anaeweza kuzuia zoezi muhimu kama hili. Na Kama kuna mtu anakuja kukuambia wewe fulani kasema, mwambie niunganishe na yeye mwenyewe.  Tumeona maene...

WADAU WAJADILI MAOMBI YA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Maimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, Mhandisi Decklan Mhaiki, akiwasilisha mambi ya shirika hilo ya kupaandishi bei ya umeme kwa asilimia 18.9 wakati wa kikao cha majadiliano baina ya wadau na uongozi wa shirika, kilichoitishwa na Mamlaka ya Udhibiti huduma za Maji na Nishati, (EWURA), na kufanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 23, 2016.   Baadhi ya viongozi wa TANESCO na wadau wakifuatilia mjadala Na K-VIS BLOG/KHALFAN SAID MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wadau wa umeme kujadili maombi ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18.9 kwa uwazi na bila hofu lakini wakizingatia nia ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga nchi yenye uchumi wa viwanda. Akifungua majadiliano ya wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zanzibar na uongozi wa TANESCO jijini Novemba 23, 2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Maji na Nishati, (EWURA), kuhusu mapendekezo hayo, Mkuu wa Wilaya ya ...

ESRF YASHIRIKIANA NA GETENERGY KUANDAA MKUTANO WA AFRIKA WA MAFUTA NA GESI

Image
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba, 21-23, 2016. Katika hotuba yake ya utangulizi, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kuwa mkutano huo umekutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya mafuta na gesi kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwepo serikali, viwanda, mashirika ya maendeleo na vyuo ambavyo vinatoa elimu ya mafuta na gesi. Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akitoa neno la utangulizi katika Mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi. "Malengo ya mkutano huu ni kuangalia changamoto gani ambazo zinalikabili Bara la Afrika katika sekta ya mafuta na gesi, kubadilisha ujuzi kwa wataalamu wa mataifa ambayo yameshiriki na kujadili hatua ya kuchukua ili kuboresha sekta hii lakini pia utasaidia kukuza ushirikiano baina ya nchi washiriki, "Katika mkutano washiriki wataisaidia Seri...