Posts

BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI

Image
 BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI #KAZIINAONGEA  Katika kuendelea  kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.   Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi. Aidha Katika vitongoji 1849 vya  Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA

Image
 SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA #KAZIINAONGEA Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa Maji kwa  wananchi wake, hivyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo ni Mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia vijiji 9 na Mradi wa Nkinga Simbo utakaohudumia vijiji 8 vilivyopo jimbo la Manonga Mkoani Tabora. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali, aliyeuliza lini Serikali itatenga Fedha za ujenzi wa Miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale - Manonga. Mhandisi Kundo amesema Mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata za Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilisha miradi hiyo. Amesema  Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa vijiji vya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika kata ya Igoweko.

SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000

Image
 SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000 #KAZI INAONGEA Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetaka gharama ya kuweka umeme kwa vijiji vyote nchini iwe ji tsh.27,000 na sio zaidi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Jijini Dodoma hivi karibuni. Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, Kapinga alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili yaweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000. Akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme ya  zaidi ya 27,000. "Kuna baadhi ya maeneo ambayo ni Vijiji yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, , namuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kufanya mapitio ya maeneo haya

MFANYABIASHARA MOSHI AGAWA MITAJI YA MIL 10 KWA MARAFIKI ZAKE .

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa bidha mbalimbali kwa kundi la Wafanyabiashara wadogowadogo walioanza Biashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya ZAC Enterprisesya mjini Moshi . Baadhi  ya Wafanyabiashara wadogowadogo katika kundi la Wamachinga 50 walionufaika na msaada kwa ajili ya kukuza mitaji kutoka kampuni ya ZAC Enterprises ya mjini Moshi  Mkurugenzi wa Kampuni ya ZAC Enterprises Izack Ngowi akioa maelezo kuhusu baadhi ya bidhaa alizokabidhi kama msaada kwa ajili ya kukuza mitaji kwa Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Wamachinga alioanza nao biashara. Baadhi ya Wafanyabiashara wakipokea sehemu ya bidhaa zilizotolewa kwao na Kampuni ya ZAC Enterprises kwa ajili ya kukuza mitaji yao  Sehemu ya msaada uliotolewa kwa Wafanyabiashara marafiki wa Izack Ngowi ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya ZAC Enterprises kwa ajili ya kukuza mitaji yao. Baadhi ya wafanyabiashara walionufaika na mtaji kutoka kwa Kampuni ya ZAC Enterprises wakiendel

“MOTO MLIMA KILIMANJARO” ,ALTEZZA WATOA VIFAA VYA MIL 210

Image
Kontena maalumu lililowekwa vifaa kwa ajili ya zoezi la uzimaji moto endapo utatokea katika Hiafadhi ya Taifa ya Kilimanjaro . Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry Andreichuk  (kushoto) akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) wakati akikabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto . Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry  Andreichuk  (kushoto) akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) wakati akikabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto  Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry  Andreichuk  akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto kwa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Baadhi ya vifaa maalumu kwa ajili ya kuzima moto katika maeneo yeny miinuko vikiwa katika kontena zilizo

MWISHAWA NAIBU KAMISHNA MPYA TANAPA

Image
ARUSHA  Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Mussa Nassoro Kuji ameongoza uapisho wa Naibu Kamishna mpya wa Uhifadhi Massana Gibril Mwishawa anayeshughulikia Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara katika Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA). Hafla ya uapisho iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA   jijini, Arusha imeambatana na uvishwaji wa cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Uhifadhi   ambapo katika salamu za Pongezi Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Musa Kuji amesisitiza uwajibikaji na kumtanguliza Mungu katika kutekeleza majukumu hayo ya Naibu Kamishna wa Uhifadhi.   ”Cheo huambatana na majukumu na uwajibikaji. Hivyo basi, ni muhimu ukamtanguliza Mwenyezi Mungu wakati wote ili aweze kukuongoza katika utekelezaji wa majukumu yako haya mapya. Taaluma, uzoefu, umahiri na kujituma kwako, kunatupatia imani kubwa kuwa utatekeleza majukumu yako kwa uadilifu, weledi, bidii kubwa na bila woga wala upendeleo” alisisitiza Kamishna Kuji   Aidha, Kamishna Kuji aliongeza kuwa katika nafasi ya Naibu Kamishna wa

"ARUSHA NI TAJIRI TUKIYAELEWA MAONO YA RAIS SAMIA"- RC MAKONDA

Image
Arusha  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda usiku wa Ijumaa Juni 08, 2024 amewasihi Waongoza watalii wa Mkoa wa Arusha kuwa waadilifu, wenye lugha nzuri na vinara wa kuutangaza vyema Ukarimu wa Watanzania kwa kila Mgeni na Mtalii watakaebahatika kumuhudumia ndani ya Mkoa wa Arusha. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa msimu wa tisa wa programu ya "Safari Field Challenge" yenye lengo la kumpata Mwongoza watalii bora wa mwaka, Shughuli iliyofanyika kwenye ukumbi wa Grand Melia Jijini Arusha ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas aliyemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki. Katika hotuba yake Mhe. Paul Makonda amewapongeza waongoza watalii hao kwa kazi nzuri akiwasisitiza kuwa wao ndiyo mabalozi wakuu wa kudhihirisha kwa vitendo kauli za Rais Samia Suluhu Hassan alizozitoa wakati wa filamu ya The Royal Tour pamoja na mahojiano mbalimbali kwenye vyombo vya habari vya