WANAWAKE WA TAASISI YA UTAFITI WA MBOGA DUNIANI WAPELEKA TABASAMU MOTONYOK ARUSHA .


WANAWAKE WA TAASISI YA UTAFITI WA MBOGA DUNIANI WAPELEKA
TABASAMU MOTONYOK ARUSHA .
Na Dixon Hussein – Arusha
WANAWAKE katika Taasisi ya Utafiti wa Mboga Duniani
“World Vegetable Center” iliyopo Tengeru jijini Arusha wame wameacha tabasamu
kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi wa kituo cha Motonyok baada ya
kukabidhi zawadi ya vitu mbalimbali ikiwemo Mchele ,Sukari,Sabuni pamoja na
nguo kama sehemu ya msaada kwa watoto hao
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa taasisi hii iliyojipambanua
katika tafiti za mboga kutumia watafiti wake kama sehemu ya maadhimisho mwezi
wa kumbukumbu ya siku wanawake Duniani,maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka
kote duniani.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa
taasisi ya World Vegetable Center Colleta Ndunguklu amewapongeza waanzilishi na
walimu wa kituo hicho kwa kutoa huduma ya malezi na elimu kwa Watoto waishio
katika mazingira magumu na wenye ulemavu.
Amesema kuwa Wanawake wa Taasisi ya World Vegetable Center wameguswa na kuamua
kutoa msaada huo kwa kuwa wanatambua mchango unaofanywa na Familia hiyo.
“Taasisi yetu inakupongeza Sana wewe na Familia yako kwa kuliona hili la
kuhudumia Watoto wenye uhitaji, Wanawake wengi wanatelekeza Watoto kwa sababu
ya kukosa uvumilivu wa kuhudumia Watoto wenye mahitaji maalumu” amesema Colleta.
“ Sisi tunatoka kwenye taasisi ya mbogamboga ,tunafanya
utafiti kwenye mboga ili kupata mbegu bora
,tunamshukuru kwa kutukaribisha hapa, tumesikia mengi kutoka kwenu pia wewe ni mama bora una mikoba mingi sana, mkoba wa kuwa mama,
mkoba wakuwa mlezi , mkoba wa kuwa mwalimu” alisema Colleta
Mkurugenzi wa kituo cha kulelea Watoto waishio katika
mazingira magumu cha Matonyo Bi. Emmy Nicholaus Sitayo amesema kituo hicho
kilianzishwa kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanyiwa baadhi
ya Watoto yatima na waishio mitaani ikiwemo ubakaji, kupigwa na kunyimwa haki
za msingi za binadamu.
Amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2006 kikiwa na
watoto tis ana sasa kinahudumia watoto waliopo shuleni Hamsini na nane ,wasichana
wakiwa ni thelathini na wavulana ishirini na nane.
“Watoto waliopo kituoni ni 58 kati ya hao 10 tayari wameshavuka wapo elimu ya Sekondari na
wengine ndo hawa tuliona nao hapa na shule
yetu ilitakiwa iwe na watoto 400 na mpaka leo tuna watoto 125”alisema Sitayo .
“Tunaamini tutafika hatuombi tupate yatima au watoto
wenye mazingira magumu tunatamani wapungue ili wawe na walezi na hapa tuna
kitengo pia cha kulea watoto wenye changamoto ya ulemavu tunawasaidia na tukisikia
mahall wanatoa elimu tunawapeleka”
aliongeza Sitayo .
Sitayo ameshukuru ujio wa taasisi hiyo katika kituo hicho
na msaada uliotolewa kwa watoto hao pamoja na elimu ya uandaaji wa shamba na
uoteshaji wa mboga jambo ambalo amelitaja kuwa ni kubwa kuwafanya watoto wajisikie
kuwa ni kundi linalo thaminika katika jamii.
“Tunaomba Muendeleze Moyo huo wa Upendo kwa Watoto wenye
uhitaji” amesema Bi Sitiya
Mwisho
Comments
Post a Comment