WANAHABARI KILIMANJARO WAPATIWA MAFUNZO YA ONLINE JOURNALISM.
Mkufunzi katika mafunzo ya uandishi wa habari wa njia ya mtandao,Bw. Lukelo Mkami akitoa maelezo kwa washiriki wa warsha hiyo inayoendelea katika ukumbi wa KNCU.
Moshi
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa
kuhakikisha wanongeza elimu juu ya mabadiliko ya teknolojia ili kuboresha kazi
zao za uandishi ziendane na mabadiliko hayo yanayokuwa kila wakati.
Hayo yameelezwa na mwezeshaji wa
mafunzo ya uandishi wa habari kwa njia ya mtandao Bw. Lukelo Mkami
yaliyoandaliwa na Muungano wa klabu za waandishi wa habri nchini(UTPC) na
kuratibiwa na klabu ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro(MECKI).
Alisema mabadiliko ya teknolijia
yanawalazimisha waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla kujifunza kila
wakati ili kuendana nayo badala ya kuendelea kutumia mifumo iliyopitwa na
wakati.
Mwezeshaji huyo alisema mabadiliko
yakitumika vyema yanaweza kubadili mifumo ya maisha ya watanzania kutoka kwenye
umaskini kwani hutoa elimu, huonyesha fursa za kibiashara na mambo mengine ya
maendeleo.
“Matumizi ya mitandao kwa baadhi ya
watanzania na hata katika nchi zilizoendelea ndio tatizo lakini siyo kwamba
kukua kwa teknolijia hakuna shida yoyote matumizi mabaya ndio yanapelekea watu
kuona mtandao unashida kubwa”alisema.
Aidha Bw. Mkami aliwaasa watanzania
kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti matumizi ya mtandao kwa watoto wao walio
chini ya umri wa miaka 18 badala ya kuingojea serikali kwani hilo ni jukumu la
kila mwanajamii ili mtandao utumike katika maendeleo zaidi.
“Ni vyema kama familia zikifanya
jitihada kwa watoto wao kujua ukuaji wa teknolojia lakini pia matumizi sahihi ya
mitandao hiyo ili waweze kukabiliana na mabadiliko hayo na siyo kuwazuia na
kungojea matamko ya serikali”alisema
Kwa upande wake katibu msaidizi wa MECKI Bw.
Dixon Busagaga aliwataka waandishi wa habari nchini kuwa mfano kwa kufanya
matumizi sahihi ya mtandao ikiwa ni pamoja kuitumia katika
kuboresha kazi zao za kila siku.
“Mabadiliko haya ni makubwa kwani
kila siku wanasayansi huibua mapya lakini tunapaswa kufuatilia, kujifunza na
kujua kwani tunashikilia nafasi kubwa katika jamii ya kuelimisha na zaidi ya
hapo”alisema
Nao baadhi ya waandishi wa habari
walioshiriki katika mafunzo hayo wameiomba UTPC kuona umuhimu wa kuongeza muda
wa kozi muhimu kama hizo ili waweze kupata elimu ya kutosha badala ya mfumo
unaotumika sasa.
Comments
Post a Comment