KIMENUKA STENDI KUU YA MABASI MOSHI,WAMILIKI WA MABASI MADOGO WAGOMA KUTOA HUDUMA.

Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma.
Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta.
Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli.
Ulinzi ukaimarishwa zaidi.
Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi.
Hata hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma kama inavyoonekana hapa.
Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi

Comments

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MREMA AENDELEA NA MIKUTANO JIMBONI KWAKE VUNJO