MTOTO WA MIAKA 9 ATAKA KUWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA KUTUMIA NJIA NGUMU.
Mzazi wa mtoto Idda Baitwa,Bw Respcius Baitwa akifanya maandalizi na mwanae ya kuanza safari ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro Mtoto Idda Baitwa akiwa na baba yake mzazi Bw Respcius Baitwa pamoja na ndugu zake wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro. Mtoto Idda Baitwa akijiandikisha katika lango la Umbwe la kupanda mlima Kilimanjaro kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima huo.nyuma yake ni Bw Respicius Baitwa akshuhudia. Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtoto Idda Baitwa ikaanza. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini. MTOTO wa miaka tisa(9) Idda Baitwa ameanza safari ya kuweka rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro akiwa na umri mdogo zaidi huku akitumia njia ya Umbwe ambayo inaaminika kuwa ngumu zaidi kwa watalii wakati wa kupanda mlima huo. Msichana huyo mwanafunzi wa darasa la nne, katika shule ya msingi Mnazi iliyoko Manispaa ya Moshi, mkoa