RAIS KIKWETE MGENI RASMI KILELE CHA MAADHIMISHO SIKU YA SHERIA NCHINI (LAW DAY)

Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande (Kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini mwaka 2015. Maadhimisho hayo yanaongozwa na maudhui yasemayo “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau”. Kushoto ni Mh. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

 Rais Jakaya Kikwete anatarijiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya sheria nchini (Law Day) itakayofanyika Februari 4, 2015, katika viwanja vya mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Othman Chande amesema kuwa maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na maudhui yasemayo  “ Fursa ya kupata haki: wajibu wa Serikali, Mahakama na wadau”.

 Amesema kwa mara ya kwanza maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya Wiki ya   Shera yatakayofanyika  katika viwanja vya Mnazi Mmoja   kuanzia  tarehe  30 Januari  2015  hadi  tarehe  2 Februari  2015 .

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/