AMUUA MKEWE NA KUFUKIA MAITI KWENYE ZIZI LA NG'OMBE.




MATUKIO ya mauaji ya kinyama yameendelea kushika kasi nchini baada ya
mkazi wa kijiji cha Ubeti wilayani Rombo, aliyefahamika kwa jina la
Peter Deogratius (43) kutuhumiwa kumuua mkewe  na kisha kufukia mwili
wake ndani ya Boma la ngombe kabla ya kutokomea kusiko julikana .



Tukio hilo la aina yake limetokea juzi ,majira ya saa 11:45 jioni
katika kitongoji cha Mreya ambapo marehemu aliyekuwa akijishughulisha
na Kilimo aligundulika kufariki dunia katika zizi hilo lililopo jirani
kabisa na chumba cha kulala watoto wake.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Geofrey Kamwela alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba marehemu alitambulika kwa jina la
Jenipher Peter(45) aliyekuwa akiishi na mumewe huyo pamoja na watoto
watatu.



Alisema mtuhumiwa mara baada ya kutekeleza mauaji hayo akiwa mafichoni
alipiga simu kwa jirani yake na kumtaarifu kuwa amemuua mkewe na
kwamba maiti ameifukia ndani ya Boma la Ng’ombe lilopo nyumbani hapo.



“Tulipata taarifa ya mauaji toka kwa jirani  yake,ambaye alidai
kupigiwa simu  na Mume wa Marehe mu kumtaarifu kuwa yeye amemuua mkewe
na maiti amefukia ndani ya boma la mifugo, ndipo  mtu huyo akaenda
kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji.”alisema Kamwela.



Alisema baada ya mwenyekiti huyo aliyefahamika kwa jina la Aloyce Swai
kupata taarifa alifika eneo la tukio na kukuta mwili wa marehemu ukiwa
umefukiwa huku kichwa kikiwa wazi na kwamba mwili wake ulipofukuliwa
ulikutwa na majeraha sehemu mbalimbali ikiwemo Kichwani .



Akitoa kumbukumbu za Mume wa marehemu huyo ,Kamanda Kamwela alisema
mtuhumiwa huyo kumbukumbu zinaonesha aliwahi kufungwa katika gereza la
Ibukoni lililopo wilayani humo kwa muda wa mwaka mmoja



Mtuhumiwa alishawahi kufungwa kutokana na kosa la kupatikana na bangi
na Pombe ya kienyeji….kwa sasa mwili Marehemu umehifadhiwa katika
hospitali ya Huruma kwa uchunguzi zaidi wa madaktari na juhudi za
kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.



Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani  hapa linawashilia watu wawili
kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya SMG ikiwa na namba 3077,
inayoaminika kutumika katika matukio mbalimbali ya kiuhalifu wa
kutumia silaha kinyume na sheria.




Kamanda Kamwela alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao huku
akiwataja kwa majina ya John Kidungure(25) na Charles Kipara(25) wote
wakiwa ni wafugaji wa kuku wilaya ya Handeni mkoani Tanga .



Alisema watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa juzi katika kijiji cha
Chereni wilayani Same, ajira ya saa 5:30 usiku baada ya kupata taarifa
kutoka kwa raia mwema aliyewashuku hao kuwa si watu wema.



”Askari walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa wanasafiri kwa
kutumia basi la kampuni ya Mtei lenye amba za usajili T883 BQR aina ya
Scania, ndipo tukaweka mtego na kulikamata gari hilo na kuwapata
watuhumiwa na baada ya upekuzi tulikuta silaha ikiwa imefichwa ndani
ya begi la nguo.”alisema Kamwela.



Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafiri kutoka mkoa wa Tanga wakielekea
Babati na kwamba jeshi hilo limeendelea kuwahoji kabla ya kufikishwa
mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.



Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/