FAMILIA YA MTOTO ALIYEGONGWA NA FUSO NA KUKATIKA MIGUU YAOMBA MSAADA WA KISHERIA.

Mama mzazi wa mtoto Felista Shirima akieleza kwa uchungu namna ambavyo mtoto wake alivyopata ulemavu wa kudumu.
Naibu Kamanda wa jumuiya ya vijana wa CCM(UVCCM) Innocent Melleck akizungumza mara baada ya kutembelea familia ya mtoto Felista wa kijiji cha Rauya Marangu wilaya ya Moshi vijijini.
Mellecky pia alikabidhi Pempers kwa ajili ya mtoto huyo.
Mama mzazi wa mtoto Felsita akitabasamu akiwa amembeba mtoto wake mara baada ya kupokea msaada wa baiskeli,Pempers na Chakula kwa ajili ya mtoto wake,hata hivyo mamahuyo bado anahitaji msaadawa kiasi sha sh Mil,1.5 kwa ajili ya malipo ya matibabu ya mtoto huyo anayodaiwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC.




Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii ,kanda ya kaskazini.


FAMILIA ya mtoto Felista Shirima (3) wa kijiji cha Rauya wilaya yaMoshi vijijini aliyepata ajali baada ya kugongwa na roli aina ya fusona kukatika miguu imeomba kusaidiwa wakili ili kusaidia kufuatiliaupya kesi dhidi ya mmiliki na dereva wa gari hilo.

Mbali na ombi hilo familia hio pia imeomba wasamalia wema kusaidiakatika kulipa deni la kiasi cha sh Mil,1.5 wanalodaiwa na hosptali yarufaa ya KCMC kama sehemu ya gharama za matibabu ya mtoto huyoaliyopatiwa katika kipindi cha miezi mitano.

Babu wa mtoto huyo ,Anord Shirima alisema mtoto huyo aligongwa wakati akimalizia kuvuka barabara ya Himo /Marangu eneo la kanisani na kusababisha mguu mmoja kukatika eneo la ajali huku mguu mwingine
ukikatwa wakati akipewa matibabu KCMC.

“Hakuna aliyeamini kuwa mtoto huyu atapona,bahati mbaya wakati wa ajali mguu mmoja ulibaki kwenye ajali,na mwingine ulikatwa wakati wa matibabu KCMC,lakini tunashukuru Mungu anaendelea vizuri ingawaje bado
kila baada ya wiki tatu tunampeleka kwa ajili ya kusafishwa.”alisema
Shirima.

Alisema baada ya tukio hilo alijaribu kufuatilia kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuona namna ambavyo suala hilo litakavyo shughulikiwa ambapo aliambiwa na jopo la wanasheria kuwa huenda gari hilo wakati
linasababisha ajali halikuwa na Bima.

“Nilifanya taratibu za kuwasiliana na mwenye chombo,niligundua mapungufu kadhaa katika chombo hicho kinachomilikiwa na Benieli Mosha huku bima ikionesha jina la mmiliki wa awali wa gari hilo ambaye ni
Nassor.”alisema Shirima.

“Kinachotusikitisha zaidi,binti mdogo kama huyu anapata ulemavu wa kudumu,na mama yake pia hana shughuli inayomuingizia kipato,familia inahitaji wakili kwa ajili ya kusaidia kufuatilia upya kesi ya mtoto
huyo.”aliongeza Shirima.

Naye mama mzazi wa mtoto Felista aliiomba jamii ya watanzania kusaidia katika malezi ya mtoto huyo huku akidai kutotendewa haki na mahakama katika kesi iliyokwisha malizika dhidi ya waliomgonga.

“Niombe ombi moja kwenu ,mtoto mekaa hospitali kwa muda wa miezi mitano na bado hajapona,ameruhusiwa kwa kupewa dhamana,nitakapokuwa nampeleka kliniki niende na kiasi cha fedha hadi deni lililopo
hospitali litakapo malizika.”alisema Beatrice.

Alisema tangu mtoto huyo alipopata ajali mmiliki wa gari hilo wala dereva hawakuwahi kumuona mtoto huyo wala kutoa ushirikiano wowote huku akiendelea kuiomba jamii kusaidia mtoto aweze kumalizia matibabu lakini pia aweze kusoma na hatima ya maisha yake iweze kujulikana.

Kutokana na hali ya mtoto huyo,naibu kamanda wa jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Innocent Melleck juzi aliitembelea familia ya mtoto huyo na kutoa msaada wa kiti cha walemavu cha Magurudumu.

“Umaskini unapomezwa na utajiri ndipo malaika kama hawa
wanateseka.nikafikiria nilipopitia mimi katika maisha yangu.nikajikuta pia nilikuwa katika maisha kama haya,nikasema tuangalie namna ya
kumsaidia huyo mtoto ili aweze kutoka sehemu kwenda sehemu nyingine”alisema Melleck.

Alisema kama mzaliwa wa eneo hilo atahakikisha kutafuta njia mbalimbali ili kuona haki ya mtoto huyo inapatikana huku akiahidi kufikisha swala hilo kwa rais Jakaya Kikwete na kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

“Rai ninayo toa kwa watanzania wenzangu ,tutazame namna ya kendesha kampeni ya kitaifa ya kuona maisha ya mtoto huyo yanakuwa salama na kuweza kupata elimu kwa umri wa maisha yake,jambo hilo liwekwe kwenye
maombi kwa mtoto huyo aliyepitiwa na fuso bado akabakia mzima.”alisema Melleck.

Mwisho.

Comments

  1. SIASA ZA MATATIZO YA WATU ZIMEANZA.....HUYO DOGO MI ALINICHUKIZA HATA MWAKA JANA TUKO KWENYE MSIBA WA BABA YA RAFIKI YANGU YEYE ALIKUWA ANAGAWA B-CARD KWA WATU WAKATI IBADA INAENDELEA...!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.