PPF YATUNUKIWA TUZO YA UBORA YA ISO KWA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA WAKE
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,
William Erio (katikati), Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Julius Mganga
(kushoto) na Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga (risk management), Ufoo Swai
wakionyesha cheti cha ubora wa utoaji huduma kimataifa kwa wananchi (ISO) wakati
wa mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam
leo Ijumaa Mei 29,
Erio akizungumzia mafanikio ambayo Mfuko umepata hadi kutunukiwa tuzo hiyo |
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio alitoa taarifa hiyo leo Ijumaa na kusema kuwa walipewa tangu Machi 28, mwaka
huu.
Alisema
wamepewa cheti chenye namba 9001:2008 na kuanzia mwezi Mei, mwaka huu huduma za
PPF zinaza kutambulika kimataifa.
“ISO
walikuja nchini wakatukagua wakalidhika na viwango vya huduma zetu tunazotoa na
wakatupatia cheti cha ubora,” alisema Erio.
Alisema
kwa sasa wanachma wa PPF wategemee kupata huduma bora pamoja na uwajibikaji
ulio bora.
Alisema
kila baada ya miezi sita ISO watakuwa wanatembelea PPF na kukagua kama huduma
bora bado zinatolewa, na kila baada ya miaka mitatu PPF watatakiwa ku-renew
maombi ya ISO.
Add caption |
Mameneja wa PPF, na waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio juu ya tuzo hiyo |
Wakurugenzi na Mameneja wa PPF |
Tuzo ya ubora ISO katika utoaji huduma kimataifa, ambayo PPF imepata |
Mameneje wa PPF, wakifuatilia kwa makini maelezo yalkiyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, kwa waandishi wa habari |
Comments
Post a Comment