Posts

Showing posts from February, 2016

BWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTOBWENI LA WAVULANA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

Image
Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana (Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3 asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna   Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. . Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa moto kwa m

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIKI AZINDUA DUKA LA HUAWEI JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa duka la simu za mkononi na huduma za matengenezo ya simu Samora jijini Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia simu orijio ili kuepuka usumbufu utakojitokeza kwa kuzimwa kwa simu feki ifikapo June mwaka huu.  Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzindizi wa duka jipya la kampuni ya huwawei mkuu wa mkoa bwana said Meck sadiki amesema kuwa zoezi la uzimaji wa simu hizo uzimaji huo haujaanzia hapa nchini bali limefanyika katika nchi nyingi zilizoendelea. Aidha Meck Sadick amesema kuwa ni wakati sasa wa makampuni ya simu kuakikisha yanatengeneza simu imara na kuwa na mafundi wa uhakika ili kupunguza usumbufu unaojitokeza kwa wateja wao.  Meneja Huawei nchini Tanzania Peter Zhangjunliang, akizungumza na wandishi wa habari hawapo picha juu ya mbinu zilizotumika na kampuni ya  Huawei, ambapo wanajitahidi  kuwa Karibu zaidi na wateja wake na k

TPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALITPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiu chumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji