MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHANDISI MATHEW MTIGUMWE AKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA PAMBA KUJADILI MAENDELEO YA KILIMO CHA PAMBA KATIKA MKOA HUO
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha
zao la Pamba katika mkoa wa Singida.
Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa pamba Mkoa wa Singida
Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini
Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika
Mkoa wa Singida
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Choro Tarimo akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo
Moja ya wakulima wa Kilimo cha pamba Wilayani Ikungi Timoth S. Nkulu akimuomba Mkuu wa Wilaya kuzisimamia Wilaya zote kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uzalishaji wa kilimo hicho.
Wadau wa kilimo cha pamba wakihakiki maazimio waliyoyapitisha
Na Mathias Canal, Singida
Zao la Pamba ni miongoni mwa mazao ya kipaombele ya biashara
yanayozaliswa Mkoani Singida kwa kuwa linastahimili hali ya hewa ya Mkoa ya
uwepo wa mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo ambapo
kutokana na hali hiyo Mkoa unaendelea kuhimiza wakulima kuzalisha zao hilo kwa
kiasi kikubwa ili waweze kuongeza kipato na usalama wa chakula.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa wadau wa kilimo
cha pamba Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew
Mtigumwe wakati akifungua Mkutano huo iliokuwa na dhamira ya kujadili maendeleo
ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa huo.
Mhe Mtigumwe amesema kuwa Katika Mkoa wa Singida Kampuni ya
Biosustain Ltd inayojishughulisha na Kilimo cha Mkataba imeweza kusaidia zao la
Pamba kwa kuanzisha kiwanda cha kuchambua Pamba chenye uwezo wa kuchambua Tani
16,000 kwa mwaka ambapo kupitia kilimo cha mkataba wakulima wa Mkoa wa Singida
wamepata pembejeo, Mafunzo ya kilimo bora na soko la uhakika ambapo katika
utekelezaji wa kilimo cha mkataba msimu wa mwaka 2015/2016 wakulima 4,204
wamepatiwa mafunzo.
Kwa msimu huu wa Mwaka 2016/2017 Mkoa umepata mgao wa mbegu
za Pamba kutoka Bodi ya Pamba jumla ya Tani 120 (Wilaya ya Iramba na Mkalama
Tani 80, Wilaya ya Manyoni Tani20 na Wilaya Ikungi na Singida Tano 20) ambazo
zinaendelea kusambazwa kwa wakulima.
Imeelezwa kuwa zao la Pamba linakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo tija ndogo katika uzalishaji (200 kg/ekari) kutokana na
wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo cha pamba, matumizi ya viuatilifu
ambavyo havina uwezo wa kudhibiti wadudu waharibifu wa zao la pamba (Feki),
Matumizi ya mbegu zisizoota vizuri (Feki), Kubadilika kwa bei ya pamba mwaka
hadi mwaka, Mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo kwa mfano
maeneo ya Bonde la Ufa ya Iramba, Mkalama na Manyoni.
Rc Mtigumwe amesema kuwa Mkutano wa wadau wa kilimo cha
Pamba ni fursa nzuri ya kuwakutanisha wadau muhimu wa zao la pamba na
kujadiliana mafaniko, Changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kufanikisha
kuongeza kwa tija na faida katika uzalishaji wa zao la pamba.
Ameeleza malengo ya kimkoa kulima zao hilo kwa kiwango kikubwa cha Hekta 8,510 kwa Mwaka 2016/2017 na
matarajio ni kuzalisha Tani 8,075.
Katika Mkutano huo kwa umoja wao wadau wa kilimo cha Pamba wamepitisha
maazimio 17 kama ifuatavyo:
- Wataalamu wa kilimo wa ofisi ya mkuu wa Mkoa na halmashauri za wilaya watafute ufafanuzi wa deni kwakushilikiana na Biosustain kumpatia Katibu Tawala wa Mkoa ndani ya mwezi mmoja.
- Katibu Tawala wa Mkoa awaandikie barua uongozi wa Kampuni ya Quton kuitwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuja kutoa maelezo kwanini hawahudhurii vikao na walete ufafanuzi wa deni wanalodaiwa na namna ya kulilipa.
- Halmashauri ya Wilaya ya Singida inatakiwa ilejeshe fedha za ushuru wa Pamba kwa halmashauri ya Ikungi iliyolipwa kwao kwa makosa ndani ya miezi sita (6).
- Elimu juu ya Matumizi ya mizani iendelee kutolewa ili kuongeza uelewa na ufanisi kwa wakulima.
- Kila halmashauri itoe taarifa ya maendeleo ya zao la Pamba kwenye eneo lake kwenye vikao vya wadau wa Pamba.
- Bodi ya Pamba ilete wakaguzi wa Pamba wasiopungua wawili kwa Mkoa wa Singida ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.
- Wakurugenzi wapitie na wasimamie mikataba inayoingiwa kati ya Makampuni na wakulima ili kuepuka malalamiko yasiyo yalazima wakati wa utekelezaji.
- CDTF wawe ni wajumbe kwenye kikao hiki na waalikwe kuanzia kikao kijacho ili watoe mchango wao kwa maendeleo ya Pamba katika Mkoa wa Singida.
9) Bodi
ya Pamba iangalie uwezekano wa kuwahusisha watafiti watoe mbegu bora inayostahimili
ukame na kutoa mazao mengi.
10) Katibu
Tawala wa Mkoa aiandikie Wizara ya Kilimo kuikumbusha kuimarisha udhibiti wa
ubora wa viuatilifu.
11) Wakurugenzi
wa halmashauri, Bodi ya Pamba na kampuni ya Biosustain waendelee kutoa Elimu
stahiki ili kukuza uzalishaji wa Pamba.
12) Kila
kaya lazima ilime ekari mbili za Pamba ili tupate Pamba yakutosha kuanzisha
kiwanda cha nguo.
13) Kila
shule ya msingi na sekondari lazima iwe na ekari mbili (2) za zao la Pamba ili
zitumike kama shamba darasa kwa wanafunzi na wananchi wanaoishi maeneo ya
jirani.
14) Wakurugenzi
wahakikishe vitabu vya mwongozo wa kilimo na mifugo vinapatikana na kuwafikia
wakulima, kila kijiji kipate nakala tano (5) kabla ya Januari, 2017.
15) Jalada la usajili lenye orodha ya wakulima na ekari zao
kiujumla na mazao wanayoyalima
Comments
Post a Comment