MOBISOL NA ZUKU TV WAZINDUA HUDUMA ZA TELEVISHENI YA SATELITE YA NISHATI YA JUA
Meneja Mkuu wa Zuku
Tv Tanzania , Bw.Omari Zuberi akiongea na waandishi
wa habari juu ya huduma mpya ya
TV ya nishati ya jua ambayo ina
channel za
Zuku Tv
katikati ni
Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens akiwa na wafanyakazi wa mobiso l katika uzinduzi huo hii
leo jijini Arusha
mmoja wa mmteja wa mobisol
ambaye akutaka kutaja jina lake akiongea wakati wa uzinduzia ambapo
aliisifia kampuni ya mobisol nakusema ni mtetezi wa wananchi wanaoishi
vijijini ambapo umeme haujafika
Meneja wa zuku Tanzania wa
kwanza kushoto akibadilishana mawazo na wa kwanza kulia ni afisa
usiano wa Zuku dada Yasta pamoja na mwakilishi wa
zuku Jack Karanja katika uzinduzi
wafanyakazi wa zuku wakifurahia
mara baada ya uzinduzi
Na Woinde
Shizza,Arusha
KAMPUNI
inayoongoza kwa utowaji wa huduma za
nishati ya jua majumbani ,Mobisol na Kampuni ya Zuku Tv inayotoa burudani za
satellite wameungana pamoja kwa ajili
kuwanufaisha watanzania wasiounganishwa na nishati ya
umeme.
Kwa pamoja kampuni
hizi zimezindua kwa mara ya kwanza TV ya nishati ya jua ambayo ina channel za
Zuku Tv huduma inayowalenga wale ambao
hawajafikiwa na umeme wa gridi ya Taifa.
Huduma hii huunganisha
mfumo wa nishati jua, televisheni ya hadi inchi 32
ya nishati jua, ungo wa satellite, na huduma ya ya kifurushi cha Zuku Smart
Plus chenye chanelli 47 and 18 za redio. Mobisol wanalenga
kutoa huduma hii kwa watanzania ambao hawajafikiwa
na huduma ya nishati ya umeme, kwa kutoa
nashati safi na ya kuaminika kwa bei nafuu popote ulipo katika mfumo moja
mkamilifu.
Mobisol inatoa vifurushi
mbalimbali vya nishati ya jua ya
majumbani, vilivyo na uwezo wa kutoa nguvu ya umeme hadi
200W, unaotosha matumizi ya kaya nzima. Kila
kifurushi kintaota paneli ya PV, betri ya nishati ya jua, taa nne za mwanga
mkali,TV kubwa ya kioo cha bapa, tochi,
chagi ya simu na redio ambayo unaweza kuichagi. Vifaa hivi vinapatikana na
waranti, huduma ya kufungiwa bure, huduma ya wateja na huduma ya marekebisho
kwa miaka 3. Pia, Kwa kuongezaTsh 8,999 kwamwezikwakifurushi,
watejawatawezakupatahudumazaZuku
TV kwamudawamasaasabakwasiku .
Akizungumza katika
uzinduzi huo Afisa masoko wa Mobisol
Sjors Martens alisema kuwa wao wanania ya kuleta maisha mazuri kwa wateja
wao nchini Tanzania.
Alisema Huduma yao ya
kifurushi cha televisheni ya satellite
kitawezesha wateja kufurahia habari , michezo, burudani na maudhui ya
elimu wakati wowote hata wakiwa wanaishi
mjini au vijijini.
Kwa upande wake Meneja Mkuu
wa Zuku Tv Tanzania , Bw.Omari Zuberi alisema
ubunifu wa huduma
hii itatuwezesha kufikia zaidi ya watanzania million 8 ambao hawajawa na
nishati ya umeme wa grid ya Taifa na kutuwezesha kuchangia kwa asilimia kubwa
ongezeko la televesheni
nchini.
“Hii ni
fursa ya kipekee na ya kuleta hamasa kwa
wateja wa Mobisol kuwa na uwanja mpana zaidi
wa kuchagua na kufurahia zaidi ya chaneli 40 za Zuku TV inayotambulika
kama huduma bora ya bei nafuu inayotoa burudani kwa
familia kwa kuhamasisha maudhui ya
kinyumbani zaidi,” alisema Zuberi.
Aliongeza kuwa Ingawa
asilimia 70 ya watanzania hawajafikiwa na huduma ya
nishati ya umeme na asilimia kubwa ya watanzania bado hawana Televisheni,
Mobisol na Zuku wametumia fursa hii na kuungana pamoja kwa ajili ya kutoa
huduma ya umeme wa jua na kutoa burudani ya TV Satellite yenye ubora wa
kimataifa
Aidha alisema kuwa
Huduma hii ya PayTV iliozinduliwa mkoani hapa itapatikana katika
mikoa ambayo
Mobisol inatoa huduma ambapo ni Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani,
Singida, Tabora, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera, Simiyu, Mbeya,
Songwe na Njombe - na baadaye kote nchini mwaka
ujao
Alibainisha kuwa Kupitia Zuku
TV, watanzania wanaweza kufurahia idadi ya
channel za kusisimua ikiwa ni pamoja na
channel za nyumbani FTA,
channel
za kimataifa na channel za Zuku
asili; Zuku Sports, hivi karibuni ilizindua tena
Zuku Swahili, Zuku Kids, Zuku Life Glam na
Zuku Nolly.
Alisema kuwa Bei ya kifurishi
cha Zuku smart pack kitakuwa kikiongezwa
kwa awamu katika mfumo nishati ya
jua ya Mobisol, ambayo wateja hulipa
kupitia simu kwa kipindi cha
miaka mitatu.
Alifafanua kuwa Baada
ya miaka
mitatu, wateja watamili hivyo vifaa na
kupata ofa ya kuvutia kwa kulipa tena huduma hiyo
mpya
Comments
Post a Comment