Posts

Showing posts from December, 2016

MKUU WA WILAYA YA ROMBO,AGNES HOKORORO AKAMATA NA KUTEKETEZA LITA 4000 YA POMBE CHAFU.

Image
Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akiangalia namna pombe ya kienyeji inavyoandaliwa baada ya kukamata kiwanda bubu cha kutengenezea pombe bila ya kufuata taratibu. Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe ya kienyeji  aliyefahamik kwa jina moja la Carlos akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo namna wanavyoandaa pombe hiyo. Carlos akifungua madumu makubwa yaliyohifadhi Pombe ya Kienyeji wakati wa utengenezaji wake katika kijiji cha Useri wilayani Rombo. Sehemu ya Pombe ikiwa katika Mapipa baada ya kuvundikwa. Kreti za Chupa za Banana ambazo zimekuwa zikitumika pia katika kuwekea pombe hiyo mara baada ya kutengenezwa. Askari Mgambo akiweka ndizi zilizovundikwa katika ndoo ambazo pia hutumika katika utengenezaji wa pombe hiyo ya kienyeji. Mkuu wa wilaya ya Rombo,Agnes Hokororo akimwaga pombe hiyo iliyokuwa katika Chupa. Mkuu wa wilaya ya Rombo Agnes Hokororo akitizama daftari la mauzo lililokutwa katika kiwanda hicho. Nyumba amba

TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA

Image
Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao. Kwa zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu yao katika wodi yao iliyopo Hospitalini hapo Muhimbili. Katika tukio hilo, Mo Dewji Foundation waliweza kutoa vitu mbalimbali kama zawadi kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho.  Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na unga wa ngano,

MBUNGE MUSSA WA JIMBO TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WAKULIMA JIMBONI MWAKE

Image
MBUNGE MUSSA WA JIMBO TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WAKULIMA JIMBONI MWAKE. Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta,Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikangalia naamna mradi huo unavyopandwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua mradi huo leo mara baada ya kuwasilia kwenye eneo hilo Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shu

EWURA YARIDHIA KWA SEHEMU OMBI LA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEME

Image
MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017. Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake. Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme. Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi. Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya

MHANDISI MAKANI ATOA WIKI MBILI KWA WAFANYAKAZI NGORONGORO KUWASILISHA TAARIFA ZA MIFUGO NA MAJENGO YA KUDUMU WANAYOMILIKI NDANI YA HIFADHI HIYO

Image
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Freddy Manongi na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto).     Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu,  ametoa wiki mbili kwa watumishi wenye mifugo na majengo ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi hiyo kujiandikisha kwa uongozi wa mamlaka hiyo ikiwa ni mkakati wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu.   Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akichangia katika mkutano huo. Alieleza kuwa salama ya Hifadhi ya Ngorongoro

ASKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU ,MLIMA KILIMANJARO.

Image
Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut. Safari ilikuwa ni usiku kucha  Jua likachomoka wakati safari ikiendelea. Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak. Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana. Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji. Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak. Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba. Safari ya kueelkea Uhuru Peak ikaendelea. Hatimaye wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga. a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiw