MGODI WA BULYANHULU WATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA WAENDESHA BODABODA MKOA WA KILIMANJARO
Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuonesha ushiriki wa mgodi huo katika maadhimisho ya wiki ya afya na usalama mahali pa kazi mwaka 2017.
Mafunzo hayo yaliyokutanisha waendesha bodaboda zaidi ya 300 mkoani Kilimanjaro yamefanyika katika ukumbi wa bwalo la polisi mjini Moshi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo alisema kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia kupitia mgodi wa Bulyanhulu inaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita ajali za barabarani.
“Katika kuadhimisha wiki ya afya na usalama mahali pa kazi mwaka 2017 tumeamua kushiriki kwa kuonesha namna tunavyozingatia masuala ya afya na usalama mgodini lakini pia kwa kuwa maadhimisho haya yanafanyika mkoani Kilimanjaro tumeona ni vyema tutoe elimu kwa waendesha bodaboda ili kupunguza n ahata kumaliza kabisa tatizo la ajali za barabarani”,alieleza Tarimo.
Tarimo alisema Dira ya Usalama ya Kampuni ya Acacia ni “Kuhakikisha kila mtu anarudi nyumbani salama na mwenye afya kila siku” hivyo kupitia mafunzo hayo ajali zitapungua.
Naye Mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mwita ambaye ni Afisa Mafunzo kutoka mgodi wa Bulyanhulu aliwataka waendesha bodaboda kujiepusha na tabia hatarishi zinazoweza kusababisha ajali ikiwemo matumizi ya vileo,mwendokasi,kutumia vyombo chakavu na matumizi mabaya ya barabara.
Mwita aliwakumbusha waendesha bodaboda kuvaa nguo za kuonekana “Reflector Vest”,kutumia vyema breki,kuendesha kwa umakini na kwa tahadhari,kuepuka kupakia abiria kama mishkaki,kutopakiza watoto wadogo na kuwa na leseni.
Kwa upande wake Ofisa Oparesheni Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro Inspekta Peter George Mizambwa aliupongeza mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na jeshi la polisi kutoa elimu ya usalama barabarani kwani suala la usalama ni la watu wote.
Inspekta Mizambwa aliwataka waendesha bodaboda kuachana na tabia ya kujaribu kuyapita magari barabarani wakiwa upande wa kushoto na kuacha kufanya mizaha wanapokuwa barabarani ili kumaliza tatizo la usalama barabarani.
Mgodi wa Bulyanhulu mbali na kutoa mafunzo pia uligawa nguo za kuonekana/kuakisi mwanga kwa waendesha bodaboda walioshiriki mafunzo hayo.
Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo Aprili 28,2017
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akizungumza wakati wa mafunzo kuhusu usalama barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akizungumza na waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akieleza namna ya waendesha bodaboda kuepuka ajali barabarani
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akizungumza ukumbini
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akiwa na maafisa kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoani Kilimanjaro
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mwita ambaye ni Afisa Mafunzo kutoka mgodi wa Bulyanhulu akitoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mwita ambaye ni Afisa Mafunzo kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiwaeleza waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro kuhusu madhara ya kutozingatia usalama barabarani
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mwita ambaye ni Afisa Mafunzo kutoka mgodi wa Bulyanhulu akionesha picha za watu waliopata ajali baada ya kukiuka sheria za barabarani
Mwendesha bodaboda akichangia mada ukumbini
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Joseph Mwita ambaye ni Afisa Mafunzo kutoka mgodi wa Bulyanhulu akijibu maswali yaliyoulizwa na waendesha bodaboda
Ofisa Oparesheni Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro Inspekta Peter George Mizambwa akiwasisitiza waendesha bodaboda kuacha kuendesha pikipiki kwa kukurupuka barabarani ili kumaliza tatizo la ajali barabarani
Ofisa Oparesheni Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro Inspekta Peter George Mizambwa akionesha namna waendesha bodaboda wanavyoendesha kwa mbwembwe barabarani matokeo yake wanasababisha ajali za barabarani
Ofisa Oparesheni Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro Inspekta Peter George Mizambwa akizungumza na waendesha bodaboda
Mwendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro akiuliza swali ukumbini
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akionesha nguo za kuonekana “Reflector Vest” kabla ya kuzigawa kwa waendesha bodaboda waliohudhuria mafunzo hayo
Afisa Rasilimali Watu mgodi wa Bulyanhulu Bryson Tarimo akiwaeleza waendesha bodaboda umuhimu wa kuvaa nguo zinazoonekana
Waendesha bodaboda mkoani Kilimanjaro wakiwa wamevaa nguo za kuonekana zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu
Waendesha bodaboda wakiwa nje ya bwalo la polisi baada ya mafunzo kumalizika
Waendesha bodaboda na maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya usalama barabarani
Waendesha bodaboda wakiwa wamevaa nguo za kuonekana wakati wa picha ya pamoja
Maafisa kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro
Picha zikaendelea kupigwa.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Comments
Post a Comment