MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAKIWA WAMELEWA WAPEWA ONYO
Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
ARUSHA-TANZANIA
Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa
wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari
hayo wakiwa wamelewa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa
Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati
akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022
katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani.
Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya
pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka
madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva.
Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe
ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama
barabarani ili kuepuka mkono wa dola.
SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa kwa makosa
hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa
kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo mbinu.
Sambamba na hilo amesema kuwa chanzo cha ajali nyingi ni ushabiki wa
mwendo kasi ambapo amewataka madereva hao kuwapuuza
wanaowashawishi kwenda mwendo kasi ili kuepusha ajali za mara kwa
mara.
Kwa upande upande wake Bw. George Emmmanuel ambae ni dereva
amelishukuru Jeshi la Polisi husasani kikosi cha usalama barabarani kwa
kutoa elimu na kuwa kuwakumbusha mambo muhimu ya kuzingatia
Barabarani.
FOOTAGE …………………………………. SP SOLOMON MWANGAMILO
Mkuu wa kikosi cha usalama
Barabarani Mkoa wa Arusha
FOOTAGE …………………………………. BW. GEORGE EMMANUEL
DEREVA
Abel Paul
Afisa Habari wa Jeshi la Paul
0759783894
Comments
Post a Comment