Posts

Showing posts from February, 2024

KAMA KIONGOZI HUFANYI KAZI YA KUMSAIDIA RAIS SAMIA HALAFU UNAIBUKA NA KUSEMA ETI MAKONDA ANAHOJI KAMA NANI, NIWAAMBIE MIMI NDIO MSEMAJI WA CCM SITAFUMBIA MACHO - MAKONDA

Image
SONGWE  "Viongozi wote iwe ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu au Ofisi yoyote ile ndani ya Nchi yetu ya Tanzania yawapasa kufanya kazi kikamilifu, wapo baadhi ya Viongozi wao wanakaa tuu maofisini Dodoma au Dar es salaam na kula viyoyozi tu, fanyeni ziara mkague watendaji wote na muache tabia ya kukombatiana na kufichiana siri" "Tembeeni na sio kusubiria CCM ikija kwenye mikutano hii mnaanza kufunga tai na kuanza kuongea ooh anaongelea sheria kama nani ? nawajibu kuwa Naongelea kama Mtanzania" "CCM tunataka kila Mwananchi ahudumiwe na sio kutishana na mimi sitishiki kabisa mnatakuwa kukumbuka kwamba hata hiyo mishahara mnayopewa ni kodi ya Watanzania" "Mimi ndio msemaji wa CCM na ninasema kwa niaba ya Mwenyekiti wetu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nimeapa nitasema ukweki bila kumung'unya maneno na kama mnadhani nitakufa sasa ..hapana Mungu wetu wa upendo bado ananihapa Afya njema" "Wapo baadhi ya Viongozi wapo Serikalini wanakula vizuri, wan

RAIA AUSTRIA AWEKA REKODI YA KUPANDA KILIMANJARO MARA 150

Image
Raia wa Austria Rudi Stangl (62) mwenye miwani (katikati) akiwa na waongoza watalii mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro kwa mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 . Raia wa Austria Rudi Stangl (62) akiwa njiani kuelekea kilele cha Uhuru Mlima Kilimajaro  Mhifadhi Vitus Mgaya kutoka idara ya Utalii (KINAPA) akimpongeza na kumvisha medali Rudi Stangl mara baada ya kushuka kutoka kilele cha Uhuru alipopanda kwa mara ya 150 .  Na Dixon Busagaga- Kilimanjaro  RAIA wa Austria Rudi Stangl (62) amejiwekea rekodi ya kupanda na kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro mara 150 akifanya kazi ya kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 ,rekodi aliyoanza kuitafuta tangu mwaka 1982 . Huenda Rudi akawa raia wa kwanza kutoka nchi ya Austria kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kuweka rekodi hii lakini pia kuwa miongobi mwa mawakala wa utalii waliotangaza vyema kivutio cha utalii cha mlima Kiliman