RAIA AUSTRIA AWEKA REKODI YA KUPANDA KILIMANJARO MARA 150
Na Dixon Busagaga- Kilimanjaro
RAIA wa Austria Rudi Stangl (62) amejiwekea rekodi ya
kupanda na kufika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro mara 150 akifanya kazi ya
kupandisha wageni kwa muda wa miaka 30 ,rekodi aliyoanza kuitafuta tangu mwaka
1982 .
Huenda Rudi akawa raia wa kwanza kutoka nchi ya Austria kuingia
kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kuweka
rekodi hii lakini pia kuwa miongobi mwa mawakala wa utalii waliotangaza vyema
kivutio cha utalii cha mlima Kilimanjaro.
Akizungumza mara baada ya kushuka lango la Marangu ,Stangl alisema
kwa mara ya kwanza anapanda Mlima Kilimanjaro ilikuwa ni mwaka 1982 akiwa na
miaka 21 akikumbuka maumivu aliyopata kutokana na kazi zote wakati wa safari ya kupanda alizifanya
mwenyewe .
“Mara ya kwanza kupanda mlima Kilimanjaro niliumia sana kwa
sababu nilibeba kila kitu mwenyewe na nilijipikia mwenyewe na nilikuwa na
tembea haraka sana ,hii ni kutokana na kwamba nilikuwa vizuri sana kwenye
michezo ila ilikuwa ngumu kufika Uhuru Peak ilikuwa tabu kwangu kufika pale”
alisema Stangl.
Alisema baada ya miaka 12 alikuja kwa mara nyingine na kundi dogo la wageni ambao ni marafiki zake kutoka
kijijini kwao na baada ya hapo ndipo akanza kufanya biashara ya kupandisha wageni
Mlima Kilimanjaro kutoka nchini kwao na sasa ametimiza miaka 30 akipanda mara ya 150.
“Kwa sasa Tanzania ni kama nyumbani kwangu kwa pili na mlima Kilimanjaro ni mlima wangu pendwa niliopanda
mara nyingi zaidi kuliko mlima mwingine hata kule kwetu Australia kama
Kilimanjaro” alisema Stangl .
Stangl alisema watu wengi wamekuwa wakishangaa anawezaje
kupanda mlima Kilimanjaro mara zote hizi na kwamba majibu yake yamekuwa ni kwa sababu anawapenda
Watanzania,analipenda taifa la Tanzania lakini pia uoto wa asili uliopo Mlima Kilimanjaro.
“Huku napenda taifa hili na penda nature ya mlima ni amazing
unajua mlima Kilimanjaro una kila kitu una hali zote unaanza kupanda mlima
kwennye eneo la nchi kavu (dry area) unaenda hadi kwenye theluji,Hakuna mlima
wowote dunia wenye nature kama hii ya mlima Kilimanjaro ,ni eneo langu pendwa
nimefika mara nyingi na penda mlima kilimanjro” alisema Stangl.
Akizungumzia tofauti iliyopo sasa katka Hifadhi ya
Kilimanjaro akilinganisha na mwaka 1982 wakati anapanda kwa mara ya kwanza Stangl
alisema kwa sasa ameshuhudia uwepo wa nyumba nyingi za kupumzika kwa wapandaji
pamoja na vyoo pamoja na umeme.
“Nature asili ya maeneo ya mlima imebadilika hili ndio kubwa zaidi theluji
imepungua kwa miaka 10 iliyopita kulikuwa na theluji nyingi kuliko sasa ,3700mts
kwa sasa kuna joto zamani kulikuwa na barafu kila mahali ninapo amka asubuhi
sijaona hili kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita sasa” alisema Stangl .
Alisema Serikali kupitia
mamlaka husika zinapaswa kufanya kitu sasa na kwamba bado kuna nafasi ya kufanya
jambo zuri zaidi kwa sababu ya watalii wengi wanakuja na kwamba Kilimanjaro
itakuwa sehemu nzuri zaidi kwa miaka 30
ijayo.
Kuhusu kuweka rekodi ya kupanda mara 150 katika kilele cha
Uhuru ,Stangl alisema imekuwa ni Fahari kwake kutimiza azma hiyo huku akitaka
ulimwengu kutambua kuhusu Kilimanjaro na kila mtu aje apande mlima Kilimanjaro .
Shirika la Hiifadhi za Taifa (TANAPA) kupitia Mhifadhi Vitus
Mgaya kutoka idara ya Utalii (KINAPA) limepongeza
jitihada zinazofanywa na Stangl katika kutangaza Hifadhi ya Taifa ya Kilimamanjaro
kwa kuendelea kupandisha wageni kutoka nchi mbalimbali kiwemo ya Austria.
“Mr Rudi ambaye ni kiongozi wa wageni “Tour Leader” amekuwa
akifanya kazi ya kuleta wageni na
kuwapoandisha katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa miaka 30 alianza kazi hii 1982 na leo
ametimiza miaka 30 ya kazi hii na ni mara yake ya 150 kufika katika kilele cha
mlima Kilimanajro.” Alisema Mgaya.
“Tunampongeza na kuwatia moyo watu wengine au viongozi
wengine wanaoleta wageni waweke rekodi zao vizuri kwa kupanda mara 100 zaidi ya
idadi aliyofanya Mr RudI tunampongeza sana” aliongeza Mgaya.
Mgaya alisema kama
Hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro wanaonelea
kuwa hili ni jambo jema na amekuwa
balozi mzuri ambaye amekuwa akitoa ushauri pindi anaposhuka kutoka mlimani akieleza
nini vya kurekebisha na mawazo yake yamekuwa yakifanyiwa kazi .
Mwisho
Comments
Post a Comment