“MOTO MLIMA KILIMANJARO” ,ALTEZZA WATOA VIFAA VYA MIL 210
Na Dixon Hussein -Kilimanjaro
VIFAA vya zaidi ya Sh Mil 200 vimewekwa katika malango sita ya kupanda na kushuka katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya mapambano ya mioto ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara katika mlima huo na kuisababishia hasara Serikali .
Kontena sita za vifaa vya kuzimia moto zimetolewa na Kampuni ya Utalii ya Altezza Taravel kwa Hifadhi ya Kilimanjaro kwa ajili ya kuwekwa katika malango ya Mweka ,Machame, Marangu na mengine yatawekwa lango la Rongai na Lemosho.
Mkurugenzi wa Alteza Dmitry Andreichuk alisema matukio ya moto katika Hifadhi ya Kilimanjaro yametoa funzo kwa wadau wa uhifadhi kuona namna bora ya kupambana na majanga ya aina hiyo kwa kuwekeza katika vifaa vya kuzimia moto.
“Kwa watu walioishi hapa ,kwa watu wanaokuja kama wageni kwa ajili ya Utalii hakika tuliona baadhi ya mambo hayajafanyika sawa na tukaona kwamba labda kuna uhitaji wa kuwa na timu yetu ya kupambana na majanga ya moto.” Alisema Andreichuk.
Alisema waongoza wageni pamoja na wapagazi katika hifadhi ya Kilimanjaro wamekuwa wakieleza changamoto wakati wa zoezi la uzimaji wa moto na zaidi walieleza kuhusu tatizo la upungufu wa vifaa.
“Watu waliojaribu kusaidia pale moto unapotokea hawakuweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kinachotakiwa kwa sababu hawana vitendea kazi hivyo kwa pamoja tuliamua kubuni kikosi cha dharura ambacho kitaifanya Hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro kuwa endelevu zaidi.” Alisema Andreichuk.
Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni ya Alteza Dickson Muganda alisema matokeo ya msaada huo yanatokana na mjadala waliofanya na Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) ya kupata vifaa kwa ajili ya dharura ya moto.
“Kama kampuni tumekaa na KINAPA na kuwa na mjadala huo tukafikia hatua ya kuwa kontena za dharura zitasaidia, kwa hiyo tukaamua kuweka kontena sita ,kontena moja kwa kila geti lenye uwezo wa kubeba watu 100.” Alisema Muganda
Alisema kampuni ya Alteza imefanya hivyo kama mchango kwa ajili ya kutunza Mlima Kilimanjaro hii ni sehemu ya ajira kwa watu wa level za aina zote wapo “Graduates” wanao maliza vyuo vikuu wanapanda kama porters ,guides wapo wanao kaa ofisini wananufaika na mlima huu pia.
“Lakini pia kwa ajili ya familia zao wale watu wanafamilia na jamii tunaona tunahitaji kujali mlima kwa ajili ya kufikia malengo ambayo serikali wameweka kufikia wageni million tano, kwa hiyo tunafanya jitihada hizi za kusaidia utunzaji wa sehemu zote zilizohifadhiwa” alisema Muganda .
Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa katika mapokezi ya vifa hivyo aliishukuru kampuni ya Alteza kwa kuja na wazo la kuwa na vifaa vya kuzima moto ka kila geti la Mlima Kilimanjaro .
“Kwa nini tulichukua hatua hizi, kwanza ni kwa sababu lazima tuchukuwe tahadhari na mlima huu unatunzwa na wenzetu wa KINAPA wanafanya kazi kubwa kupitia mtendaji mkuu na timu yake “.alisema Mkalipa
“Lakini kuna jamii inazunguka kwenye mlima huu kuna wilaya nyingi Siha,Moshi, Hai, Rombo na maeneo mengine yanayozunguka mlima huu kwa hiyo ukiangalia kwenye mlima huu tumeweka kontena moja kila geti ambayo yametolewa na wenzetu wa Alteza .
Kwa upande wake Mkuu a Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Angela Nyaki alisema msaada huu umepatikana kutoka kwenye kampuni ya Altezar,Kampuni ambayo imekua msaada wakati wote majanga ya moto yanapotokea.
“Wamekuwa wakitoa watumishi wao kwa ajili ya kwenda kusaidia kuzima moto lakni baadae wakaona ni umuhimu tukajadilina pamoja kwenye vifaa kwa sababu changamoto kubwa ina kuwa kwenye vifaa ndipo wakatengeneza hizi kontena na wakaweka na vifaa ambavyo ndio vifaa mara nyingi asilimia 90% ndio vinatumika kwenye kuzima moto.” Alisema Nyaki
“Tunawashukuru sana ingawa tunaomba mioto isitokee lakini inayotokea lazima kupambana nayo kwa hiyo mnaona vifaa hapa tuna mashoka majembe na moto wa Kilimanjaro mara nyingi ndo vifaa vinavyotumika kwa sababu unakuwa inatoka chini kwa chini kwa hiyo unapokuwa na majembe unakuwa kama unauvuruga unazima”aliongeza Nyaki .
Kampuni inayofanya shughuli za Utalii ya Alteza ya mkoani Kilimanjaro ndio wamekuwa wadau wa kwanza kutoa kontena sita zilizosheheni vifaa mbalimbali vikiwemo mashine ya kukata miti (Chain saw),majembe ,mashoka na koleo.
Mwisho
Comments
Post a Comment