RC MAKONDA AAGIZA POLISI KUTOSIMAMISHA MAGARI YA UTALII BARABARANI

 

Ataka Teksi zote kuwa na rangi ya kufanana 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kutokukamata magari ya Utalii kwenye Mkoa wa Arusha na badala yake ukaguzi kwa watalii ufanyike kwenye mipaka na kwenye viwanja vya ndege vinavyotumika na watalii.

Mhe.Makonda amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo Juni 08, 2024 kwenye Viwanja vya Magereza Kisongo, Ikiwa ni siku ya ya maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu Kili Fair 2024, yakijumuisha makampuni zaidi ya 700 ya kimataifa kutoka kwenye mataifa zaidi ya 50.

Katika hatua nyingine pia Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa miezi miwili kwa magari (Teksi) zinazotumika kubeba wageni na watalii wa Mkoa wa Arusha kuwa na rangi maalumu za kufanana ili kutoa  urahisi kwa mtalii kulifahamu gari husika pamoja na kutoa hakikisho la usalama kwa wageni na watalii wanapoamua kutumia aina hiyo ya usafiri wawapo Jijini Arusha.

Mhe. Makonda amechukua hatua hiyo ili kuendelea kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na ukarimu wa Watanzania akitaka kila mmoja kwenye eneo lake la kazi kuonesha ukarimu huo kwa vitendo kila wanapokuwa wanahudumia wageni.

                Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa kutimiza maelekezo yake hayo kutasaidia kutowapotezea muda mrefu watalii wawapo njiani suala ambalo litawapa muda zaidi wa kuwepo kwenye hifadhi za utalii na sehemu nyingine, suala litakaloongeza muda wa matumizi ya fedha,bidhaa na huduma nyingine zinazopatikana Mkoani Arusha na hivyo kuingizia mkoa fedha nyingi zaidi za kigeni.

Comments

Popular posts from this blog

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/