MFANYABIASHARA MOSHI AGAWA MITAJI YA MIL 10 KWA MARAFIKI ZAKE .
Na Dixon Hussein- Moshi
MFANYABIASHARA Izack Ngowi kupitia kampuni yake ya ZAC Enterprises
ametoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwa lengo
la kuwaongezea mitaji wafanyabiashara wadogo maarufu kama Wamachinga 50 wa
mjini Moshi aliokuwa nao wakati wakianza biashara pamoja.
Izack ametoa msaada huo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Nurdin Babu ikiwa ni sehemu ya kampuni yake kurejesha sehemu ya faida kwa jamii
hususani wafanyabiashara hao ambao wamepatiwa vifaa vya thamani ya sh Mil 10.
“Nimelenga kufanya hivi kwa kuwa mimi hapo kabla pia
nilikuwa Mmachinga kama nyie kwa hiyo katika harakati zangu za biashara nikaona
ni vyema na mimi niwashike mkono Wamachinga au wafanyabiashara wadogowadogo”
alisema Izack.
“Nafanya hivi ili kuongeza mahusianao kati ya brand (Chapa)
yetu na wafanyabiashara wadogo wadogo
wamachinga lakini vile vile nimependa kufanya hivi ili kuwaonesha fursa
kwamba katika brand (Chapa) yetu ya Zac tuna product ndogo ndogo hizi ni
biashara ambazo nyie mnaweza mkafanya ymlango kwa mlango.” Aliongeza Izack.
Alisema lengo jingine la kutoa msaada huo ni kutoa hamasa
kwa kundi hilo ili kesho waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa ambao wataweza
kuwainua vijana wenzao kiuchumi kwa
kuwaajiri na kupunguza kundi la vijana wasio na ajira.
“Nimefanya hivi kutoa hamasa ,leo nyie ni wamachinga lakini
kesho mnaweza mkawa wafanyabiashara
wakubwa ,wafanyabiashara wote wakubwa kunasehemu walitoka ,walianzia wakafanya kazi kwa bidi wakatengeneza
mahusisno mazuri na watu wakapata mitaji wakawa wakubwa” alisema Izack.
Akiizungumza baada ya kukabidhi msaada huo ,Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Nurdin Babu aliyekuwa mgeni rasmi amepongeza hatua ya mfanybiashara
Izack kukumbuka uhitaji wa vijana wenzake katika kujikwamua kiuchumi
“Kutoa ni moyo na wala sio utajiri ameeleza hapa kwa kifupi
kwamba yeye alikuwa miongoni mwa wamachinga ambao na yeye anatembeza vitu
barabarani kwa hiyo ametembeza kwa malengo akawekeza kidogo kidogo hatimaye leo
amekuwa mfanyabiashara wa kati “alisema Babu .
“Izack ameamua kumuunga mkono Mh Rais kwa vitendo na ndugu
zangu kutoa mtaji wa milioni kumi kwa ajili ya kuwakabidhi nyinyi ndugu zake
ambao mmeanza naye kazi ,yeye Mungu
akamjalia akafika hatua aliyofika sio jambo rahisi inataka moyo sana.” Aliongeza Babu.
Alisema mfanyabiashara Izack kaamua kutoa vifaa vya milioni 10
kwa ajili ya kuwapa ndugu zake ambao walihangaika pamoja ni jambo la nadra sana
kuona watu waliofanikiwa ama wafanyabiashara wanawakumbuka watu walioanza nao.
“Kwa hivyo nataka muige sasa yeye anatoa vifaa vya milioni
kumi na nyie ambao mnafanya biashara pamoja na ile mitaji yenu hakikisheni sasa
mnaweka mitaji yenu vizuri ili nanyie mmfikie kama alivyofika yeye.” Alisema Babu.
Aidha Babu alipongeza hatua ya wafanyabiashara wa mkoa wa
Kilimanjaro kuendelea na biashara zao bila ya kufunga maduka na kwamba hata
kama zipo changamoto zinazowakabili serikali itaendelea kuzitatua kwa wakati.
“Ndugu zangu nyie mnajitafutia riziki kwenye maeneo mbali
mbali na hatutaki serikali kuwabugudhi lakini na nyie lazima mtii sheria bila
shuruti yani mkiambiwa hapa ndio maeno ya wafanyabiashara ndogondogo wamachinga
basi mjue ndio hapo hasa mkiondoka mkienda kwenye maeneo mengine ndo ugomvi”
alisema Babu .
“Juzi miliona watu wa Musoma mliona sasa hayo siyataki
kwneye mkoa wangu wa Kilimanjaro nataka mkiambiwa mfanyebiashara hapa basi
mtiii lakini changamoto zenu DC amezisema naye ndio mkuu wenu wa wilaya
atazishuhghulikia kama kuna jambo amablo nyie mnaona je serikali imewapa eneo
ambalo halifikiki na wananchi hawafiki hamfanyi biashara DC atatafuta utaratibu
mwingine “ ALIONGEZA babu.
Naye mkuu wa wilaya ya Moshi Zephania Sumari amesema tayari
wamepanga kukutana na kundi la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama
Wamachinga ili kuangalia namna gani wanaweza kutatua changamoto zilizopo na
kuzipatia ufumbuzi.
“Nimeweza kukutana na ninyi wafanayabiashara wadogo wadogo
maarufu kama Wamachinga ,Mh Mkuu wa mkoa hawa sio wageni kwangu nimeshakutana
na viongozi wao wa mkoa nimekutana na viongozi wao wa wilaya na waliongea
baadhi ya changamoto nina furaha kukujulisha kwamba hawana changamoto nyingi “alisema
Babu.
Kampuni ya ZAC Enterprises inayosambaza vifaa mbalimbali vya
umeme pamoja na simu za mkononi tayari imekabidhi vifaa hivyo kwa walengwa
ikiwa ni awamu ya kwanza na kwamba itaendelea na utaratibu huo mara kwa mara .
Mwisho .
Comments
Post a Comment