BILIONI 4 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KONDOA ,DC NYANGASA AONYA

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa Bi Dollah Kilo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi na vyanzo vya maji katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akiwa ameongozana na watendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira pamoja na Ruwasa Kondoa alipotembelea ofisi mpya za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa .

Sehemu ya miundombinu ya maji kwa ajii ya ukamilishaji wa mradi mkubwa wa Maji wa Bilioni nne uliotolewa na Serikali kwa ajili ya kunguza changamoto ya Maji kwa wananchi wa wilaya ay Kondoa .
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akioneshwa jambo na Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kondoa Mhandisi Merinyo wakati wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji .

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa Bi Dollah Kilo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi na vyanzo vya maji katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa Bi Dollah Kilo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi na vyanzo vya maji katika wilaya hiyo.

Na Mwandishi wetu - Kondoa 

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt ,Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni nne imetolewa ili kuondoa kadhia ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma .

Mkuu wa wilaya ya Kondoa Fatuma Nyangasa ametembelea na kukagua miradi na vyanzo vya maji katika wilaya hiyo akieleza kuwa kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 75 huku ukitaraji kukamilika ifikapio mwezi Juni mwaka huu .

Amesema kwa sasa Kondoa inapata huduma yam aji kwa asilimia 68 pekee na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaongeza uzalishaji wa maji na kupounguza changamoto kwa wananchi wa maeneo hayo huku akionya wananchi wenye tabia ya kuharibu miundombinu ya maji hatua kali zitachukuliwa dhidi yao 

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Kondoa Dollah Kilo amesema wamejipanga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika wilaya hiyo huku akiomba ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa wale wenye kufanya vitendo vya kuharibu miundombinu ya maji pamoja na vyanzo .

Comments

Popular posts from this blog

TIB YAKABIDHI MICHORO HALISI YA KITUO CHA MABASI KWA UONGOZI WA MANISPAA YA MOSHI.

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU UPOTOSHAJI JUU YA SARAFU YA SH ,500/