Posts

WAKUTANA KUJADILI MKAKATI WA MRADI WA KIJIJI CHA DIGITALI

Image
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali. Na Mwandishi wetu, Bagamoyo WADAU mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi kuwa na tija kwa wananchi wake. Yusuph alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitatu. Alisisitiza kwamba kwa kuwa mradi huo uta...

MKURUGENZI WA TAMWA ATUNUKIWA TUZO YA CEFM CHAMPION

Image
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mh. Alexandre LĂ©vĂŞque akimkabidhi tuzo ya kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,Bi. Valerie Msoka kwa kufanikisha kampeni dhidi ya ndoa za utotoni.(Picha zote kwa hisani ya mtandao wa hivisasa.co.tz ). Na modewjiblog team Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka, amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya CEFM Champion, na Ubalozi wa Canada nchini. Katika sherehe fupi iliyofanyika Serena Hotel 24 Februari 2015, Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre Leveque alisema kuwa Valerie Msoka amekuwa mwanaharakati wa kwanza kutunikiwa tuzo hiyo na ubalozi wake kama ishara ya kukubali mchango wake kupiga vita ndoa za utotoni, za kulazimishwa na ukeketaji kwa watoto wa kike nchini. “Watoto wa kike na wanawake wamevumilia machungu ya ndoa za utotoni na za kulazimishwa hivyo wanahitaji mtu wa kuwasemea: mtu ambae ataelezea taarifa zao zinakazosaidia kuwaweka watu pamoja na kuleta mabad...

MUIGIZAJI CHUCHU HANS AZIRAI NDANI YA JENEZA AKIIGIZA.

Image
Chuchu Hans amejikuta akizirai ndani ya jeneza wakati akiigiza sini ya kifo kwenye filamu. Chuchu alikumbwa na hali hiyo hivi karibuni akiwa ‘lokesheni’ ya kuigizia filamu hiyo maeneo ya Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam ambapo sanjari na yeye, msanii mwingine aliyecheza nafasi ya mwanakwaya naye alipoteza fahamu wakati kipande hicho kikirekodiwa. Chanzo kimoja kutoka ndani ya kundi la wasanii waliokuwa wakiigiza filamu kililiambia Gazeti la Amani  kuwa, Chuchu alikumbwa na hali hiyo kutokana na wasiwasi na ujasiri wa kuuvaa uhusika. “Awali, Chuchu alionesha wasiwasi wa kuigiza kipande hicho cha kumwonesha yeye yumo ndani ya jeneza akiwa amefariki dunia kwa ugonjwa kama wa kichaa kilichotokana na msongo wa mawazo baada ya kubakwa. “Mbaya zaidi, mwongozaji naye alisema ni lazima akiwa amelala ndani ya jeneza awekewe pamba za kuziba matundu ya pua kama maiti wanavyowekewa,” kilisema chanzo. Chanzo kikazidi kudai kwamba, taharuki yote hiyo ilitokea pale, ‘mwili’ wa Chu...

Tizama:AZAM FC WAPOKELEWA NA GARI LA KUBEBA TAKA ZA KLABU YA EL MEREICK.

Image
 Hili ndilo basi ambalo El Merreikh wamewapatia Azam FC baada ya kuwasili Khartoum Basi aina ya Coaster ambalo wamepewa Azam FC Sudan WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Azam FC wamepata mapokezi ya ‘kigaidi’ mjini Khartoum , Sudan baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya mchezo na wenyeji, El Merreikh. Kwanza , walipotua Uwanja wa Ndege, wachezaji na msafara mzima walianza kufanyiwa vitimbi na watu wa Idara ya Uhamiaji katika kupatiwa visa za kuingia nchini humo. Baada ya kuufuzu mtihani huo, walikutana na visa zaidi walipotoka nje ya Uwanja wa Ndege, kufokewa na watu waliokwenda kuwapokea, kabla ya kwenda kuwapakia katika basi bovu na baya aina ya Coaster. Pamoja na hayo, Azam FC kwa kuwa walijua watakutana na hali kama hiyo, hawakuonekana kustaajabu, badala yake kuvumilia yote.   Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu kutoka Khartoum kwamba wamefanyiwa mambo ambayo kwa u...

SUMMARY OF IMPORTANT DETAILS FOR KILIMANJARO MARATHON

KILIMANJARO MARATHON 2015 (13 th Edition) SPONSOR SPONSORSHIP PRIZE MONEY OTHER PRIZES ENTRY FEES STARTING TIMES Kilimanjaro Premium Lager Main sponsors /Kilimanjaro Premium Lager 42.2km Marathon 20 million (Total) 1 st 4m/=, 2 nd 2m/=, 3 rd 1m= 4 th 900k 5 th 600k 6 th 400k 7 th 350 8 th 300k 9 th 250k 10 th 200k Medals and T-shirts will be available to the first 300 finishers. Foreign residents: $60 / East African citizens Tsh6000 / East African residents or work permit holders $30 Registration on 27 th Feb and 28 th Feb from 10am to 5pm at Keys Hotel 6.30am at Stadium Tigo Half Marathon 10 million (Total) 1 st 2m/= 2 nd 1m/= 3 rd 500k 4 th 450k 5 th 300k 6 th 200k 7 th 175k 8 th 150k 9 th 125k 10 th 100k Medals and T-shirts will be available for the first 2800 finishers. ...

PUSH MOBILE, UN , WIZARA KUKABILI EBOLA

Image
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Push Mobile, Freddie Manento (kushoto) wakitiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa kutoa elimu kwa jamii kupitia ujumbe mfupi maneno katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mratibu mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa jijini Dar. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dkt. Jama Gulaid.(Picha na Umoja wa Mataifa). Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya simu ya Push Mobile imetiliana saini na serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) ya kuwafikia watu milioni 10 ikiwahabarisha kuhusu ugonjwa hatari wa ebola. Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mjini hapa kampuni hiyo ya simu imesema kupitia ushirikiano huo kampuni hiyo ya simu itaunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa wa kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo uj...

MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA MH TEMBA NAYE AFIKISHWA KWA PILATO.

Image
Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa Nipashe, Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo. Mheshimiwa Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe. Aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai. Akisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion Iiliyopo Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma ki...