Tizama:MSAFARA WA MAGARI YASIYO NA IDADI YALIVYO PAMBA HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI.

Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya
Ng'ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa
ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.

Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .

Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel Nassari akimpongeza mwanae kwa hata hiyo.
Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.
Maharusi wakaaga katika viwanja vya Kanisa la Kilenga .
Bi Harusi Anande Nnko akiwa katika gari tayari kuelekea katika viwanja vya Usa-River Academy.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko
wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la
Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya  Usa-River
Academy.

Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.
Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.
Mharusi waki "Show Love"
Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao .
Barabarani kulijaa watu wakimshangilia Mbune wao akijinyakulia Jiko.
Kama kawaida Jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili.
Msafara wa magari ulikuwa ni mrefu .
Madereva wa boda boda pia walikuwepo kuongoza msafara .
Wananchi hawa jamii ya Maasai walitembea umbali mrefu na msafara huku wakiimba nymbo na hatimaye msafara ukaingia Ngurdoto Mountain Lodge kwa ajili ya upigaji wa picha .
Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini alikuwa katika sherehe hiyo matukio mbalimbali mtaendelea kuyapata hapa na http://dixonbusagaga.blogspot.com.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

MAKATIBU WA CCM VUNJO WASEMA HAWANA UGOMVI NA KATIBU WAO WA WILAYA.