Posts

Showing posts from May, 2018

WALIOKAIDI KUHAMA KWENYE MAENEO YENYE MAFURIKO SAME SASA KUKAMATWA

Image
Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko . Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini. Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao. Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia. Na hizi ndio sehemu za makazi ya wananchi hawa. Huduma Muhimu kama Choo zimeanza kujengwa katika eneo hilo. Wananchi Jamii ya Massai pia ni miongoni mwa waathirika wa Mafuriko hayo. Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana  na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali. Baadhi ya Nyumba za Jamii ya Kimasai zikianza kujengwa kati

MAFURIKO SAME YAKATA MAWASILIANO YA MIOUNDO MBINU ,WANACHI WATUMIA MITUMBWI NA TREKTA KUSAFIRISHA MALI ZAO.

Image
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (aliyenyoosha mkono) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Maafa  ya mkoa wakiwa eneo la Ruvu Darajani ambako magari yanaishia baada ya miuondo mbinu ya barabara kujaa maji . Moja ya barabara ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakazi wa maeneo ya Ruvu Muungano na Darajani ikiwa imejaa maji na kusababisha adha kwa wasafiri. Baadhi ya wananchi wakijaribu kuyahama makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji katika Vijiji vya Ruvu  Marwa na  Ruvu Mferejini. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia usafiri wa pikipiki kwa maeneo ambayo bado hayajafikwa na maji mengi. Kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika vibaya baadhi ya wafanyabiashara ya bidhaa ndogondogo wametumia kadhia hiyo kununua bidhaa kama Unga na Mchele na kuwauzia wananchi waliozingirwa na maji kwa bei ya juu. Usafiri pekee kwa sasa katika maeneo hayo ni Trekta na Mitumbwi ambayo imekuwa ikitumika kuhamisha mali pamoja na wananchi. Na Hii ndio hali Hal

KATIBU TAWALA MKOA WA KILIMANJARO,MHANDISI AISHA AMOUR AONGOZA WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA KUTEMBELEA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour akiwa ameongozana na wajumbe wengine wa Kamati ya Maafa kutembelea Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga ambalo linatajwa ujazo wake wa  maji  wa kawaida umepitiliza na kusababisha  Mafuriko kwa wakazi waishio kando ya Bonde la Mto Pangani. Mhandisi ,Aisha Amour akitizama kina cha Maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kilichofikia Mita za ujazo 689.88 . Sehemu ya Bwawa la Nyumba ya Mungu. Baadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu wakitumia usafiri wa Mitumbwi kusafiri kutoka upande mmoja kwenda upande wa Pili. Sehemu ya Mapitio ya Maji baada ya kujaa katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ,maji haya yanaelekea katika maeneo ambayo yapo makazi na mashamba ya watu yaliyopo pembezoni mwa Bonde la Mto ,Pangani. Maji yakiendelea kuenea katika uwanda wa Tambarare baada ya kujaa Bwawa la Nyumba ya Mungu. Na Dixon Busagaga wa Gobu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAZINDUA KITUO CHA KUTOA MSAADA WA KISHERIA

Image
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro Prof Lughano Kusiluka  akisisitiza jambo kwa wanafunzi chuo hicho kitivo cha Sheria alipowataka kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi mara baada ya uzinduzi wa kituo cha Sheria chuoni hapo   Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mohamed Utaly aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kituo cha Msaada wa kisheria katika Chuo Kikuu cha  akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanzishwa kwa kituo cha msaada wa kisheria chuo kikuu Mzumbe Mkoani Morogoro anayefata alieshikilia vitabu ni  makamu mkuu wa chuo kikuu cha mzumbe Prof, Lughano Kusiluka

WABUNGE WA MIKOA YA KUSINI WAIMWAGIA SIFA SERIKALI NA TANESCO KWA KUMALIZA KERO YA UMEME MTWARA NA LINDI

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, (wane kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi, na Mkuriugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, wakati alipowasili kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018. Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akitoka eneo la mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme wa Megawati 4 kila mmoja baada ya kuizindua, kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi Mkoani Mtwara Mei 21, 2018. Wabunge wa Mikoa ya Kusini, wakiwa na mwenyekiti wao, Mhe. Selemani Bungara(wapili kushoto)   NA MWANDISHI WETU, MTWARA-MEI 22, 2018 WABU