Posts

EFTA KUONGEZA IDADI YA WATUMIAJI WA TREKTA

Image
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw. Dustan Kyobya akizungumza na wakulima wa wilaya ya Kilombero, na kuwahimiza kutumia zana bora za kilimo ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyokuwa yameandaliwa na taasisi ya EFTA inayojihusisha na utoaji wa mikopo ya mashine za kilimo kwa wakulima. Baadhi ya wakulima wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wakati wa mafunzo hayo. Afisa Masoko na Mauzo wa kampuni ya kilimo ya Hughes ya Jijini Arusha, inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa matrekta aina ya New Holland hapa nchini Bwana Boniface Mollel (Katikati), akitoa maelekezo kuhusu trekta za New Holland TT75, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EFTA Bwana Nicomed Bohay (kulia) wakati wa mafunzo ya siku moja ya kilimo bora kwa wakulima wa wilaya ya Kilombero, wengine katika picha ni Bwana Leonce Malamsha (kushoto) Afisa Uendeshaji Mkuu wa EFTA. Afisa Uendeshaji Mkuu wa EFTA (aliyekaa) Bwana Leonce Malamsha akimsajili mmoja wa washiriki walio...

MADEREVA WANAOENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAKIWA WAMELEWA WAPEWA ONYO

Image
Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi ARUSHA-TANZANIA Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022 katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani. Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva. Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka mkono wa dola. SP Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye kamatwa kwa makosa hayo atafungiwa leseni yake na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa kuhatarisha Maisha ya watu na uharibifu wa miundo mbinu. Sambamba na hilo a...

WALIOKAIDI KUHAMA KWENYE MAENEO YENYE MAFURIKO SAME SASA KUKAMATWA

Image
Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko . Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini. Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao. Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia. Na hizi ndio sehemu za makazi ya wananchi hawa. Huduma Muhimu kama Choo zimeanza kujengwa katika eneo hilo. Wananchi Jamii ya Massai pia ni miongoni mwa waathirika wa Mafuriko hayo. Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana  na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali. Baadhi ya Nyumba za Jamii ya Kimasai zikianza kujengwa ...

MAFURIKO SAME YAKATA MAWASILIANO YA MIOUNDO MBINU ,WANACHI WATUMIA MITUMBWI NA TREKTA KUSAFIRISHA MALI ZAO.

Image
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (aliyenyoosha mkono) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Maafa  ya mkoa wakiwa eneo la Ruvu Darajani ambako magari yanaishia baada ya miuondo mbinu ya barabara kujaa maji . Moja ya barabara ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakazi wa maeneo ya Ruvu Muungano na Darajani ikiwa imejaa maji na kusababisha adha kwa wasafiri. Baadhi ya wananchi wakijaribu kuyahama makazi yao baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji katika Vijiji vya Ruvu  Marwa na  Ruvu Mferejini. Baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia usafiri wa pikipiki kwa maeneo ambayo bado hayajafikwa na maji mengi. Kutokana na miundombinu ya barabara kuharibika vibaya baadhi ya wafanyabiashara ya bidhaa ndogondogo wametumia kadhia hiyo kununua bidhaa kama Unga na Mchele na kuwauzia wananchi waliozingirwa na maji kwa bei ya juu. Usafiri pekee kwa sasa katika maeneo hayo ni Trekta na Mitumbwi ambayo imekuwa ikitumika kuhamisha mali pamoja na wananchi. Na Hii...

KATIBU TAWALA MKOA WA KILIMANJARO,MHANDISI AISHA AMOUR AONGOZA WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA KUTEMBELEA BWAWA LA NYUMBA YA MUNGU

Image
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour akiwa ameongozana na wajumbe wengine wa Kamati ya Maafa kutembelea Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga ambalo linatajwa ujazo wake wa  maji  wa kawaida umepitiliza na kusababisha  Mafuriko kwa wakazi waishio kando ya Bonde la Mto Pangani. Mhandisi ,Aisha Amour akitizama kina cha Maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kilichofikia Mita za ujazo 689.88 . Sehemu ya Bwawa la Nyumba ya Mungu. Baadhi ya wakazi wa vijiji vya jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu wakitumia usafiri wa Mitumbwi kusafiri kutoka upande mmoja kwenda upande wa Pili. Sehemu ya Mapitio ya Maji baada ya kujaa katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ,maji haya yanaelekea katika maeneo ambayo yapo makazi na mashamba ya watu yaliyopo pembezoni mwa Bonde la Mto ,Pangani. Maji yakiendelea kuenea katika uwanda wa Tambarare baada ya kujaa Bwawa la Nyumba ya Mungu. Na Dixon Busagaga wa Gobu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.