Posts

Showing posts from March, 2014

WATOTO WA FAMILIA MOJA WATEKETEA KINYAMA KWA MOTO TABORA MJINI.

Image
amanda wa Polisi wilaya ya Tabora  OCD  Samwel Mwampashe akizungumza na wananchi wakati wa tukio hilo la kusikitisha lililotokea na kupoteza maisha ya watoto hao. Chumba ambacho watoto hao walipokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambao chanzo chake inadhaniwa kuwa ni hitilafu za umeme. Miili ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8)na mdogo wake Emmanuel Paul(3) ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani majira ya saa moja asubuhi huko eneo la mtaa wa Rufita Mwanzaroad Tabora mjini. Katikati alijishika kichwani ni Paul Daniel ambaye baba wa watoto hao walipoteza maisha akiangalia maiti za watoto wake hao wawili muda mfupi mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo maswali mengi yalizuka baba huyo alikuwa wapi wakati watoto wanateketea kwa moto ndani ya nyumba. Baadhi ya wananchi wakichungulia dirishani wakiangalia namna watoto walivyoteketea kwa moto Majonzi makubwa kuhusiana na kifo ch

KIMENUKA STENDI KUU YA MABASI MOSHI,WAMILIKI WA MABASI MADOGO WAGOMA KUTOA HUDUMA.

Image
Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma. Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta. Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli. Ulinzi ukaimarishwa zaidi. Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi . Hata hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma kama inavyoonekana hapa. Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi

makala maalum MUWSA.

Image

SAFARI LAGER NYAMA CHOMA ,BAA YA MAKANYAGA YAIBUKA KIDEDEA

Image
Mwakilishi wa Baa ya Makanyaga, Rogarth Frimini Massawe (aliyeshika kombe) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Bia ya safari lager akiwemo Meneja wa Bia hiyo, Oscar Shelukindo (wa tatu kushoto waliosimama), baada ya kutawazwa mabingwa wapya wa Moshi katika shindano la safari lager nyama choma 2014. Mchoma nyama mkuu wa Baa ya Makanyaga akishangilia ubingwa wake katika shindano la mwaka huu la Safari Lager Nyama choma 2014. </ tr> Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro (RPO), ACP Hamis Nkubasi, akimkabidhi Mchoma nyama mkuu wa baa ya Makanyaga, Rogarth Frimini . Mwakilishi wa Baa ya Forest, Thadeus Mushi (kushoto)akishangiliana mfanyakazi mwenzake baada ya kuibuka mshindi wa pili katika shindano la mwaka huu la Safari Lager nyama choma 2014, mjini Moshi. Mwakilishi wa Baa ya Forest, Thadeus Mushi (katikati) akipokea fedha taslim shilingi laki nane kutoka kwa Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro (RPO), ACP Hamis Nkubasi, wanaoshuhudia ni Me

POLISI YANASA KIWANDA CHA KUTENGENEZA KONYAGI FEKI

Image
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitizama sehemu ya mbele ya kiwanda cha kutengenezea Konyagi feki ambapo muonekano wake ni maduka na saloon. Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitembelea sehemu ya nyuma ya kiwanda cha kutengeneza Konyagi feki katika eneo la kambi ya raha Bomang'ombe wilayani Hai. Sehemu ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda hicho zikiwa kituo cha polisi Bomang'ombe. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha Pombe feki ya Konyagi  iliyokamatwa hivi karibuni wilayani Hai Kamanda Boaz akiwa ameshikilia sehemu ya malighafi zinazotumika kutengezea Konyagi Feki. Kamanda Boaz akionesha mihuri ambayo imekuwa ikitumika kuonesha tarehe ya kuanza na kumalizika kwa tarehe ya matumizi ya kinywaji hicho. Kamanda Boaz akitizama Ndoo kubwa maarufu kama Diaba ambayo yamekuwa yakitumika kuchuja pombe hiyo kabla ya kuwekwa katika karatasi maalum. Hivi ndivyo inavyoonekana pombe hiyo ikiwa na