Na Mwandishi wetu. OFISI ya mkurugenzi wa Mashtaka Nchini imemfutia mashtaka ya mauaji,mmoja kati ya watuhumiwa nane wa mauaji ya kukusudia dhidi ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite bilionea , Erasto Msuya (43). Hati ambayo imetumika kumwachia huru Joseph Damas (Chusa) ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa madini hayo imetolewa na kusainiwa na mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Elieza Feleshi na kisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuiwasilisha kwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Munga Sabuni . Hati hiyo ambayo hufahamika kama “Nolle Prosecution “ilitolewa mbele ya mahakama hiyo April 16 mwaka huu kwa ajili ya kuingiza rasmi katika kumbukumbu za Mahakama. “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii, umekamilika na ikikupendeza, upande wa mashitaka tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya mashahidi kabla ya kulipeleka jalada lenye mashitaka haya, Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia