Posts

Showing posts from June, 2024

“MOTO MLIMA KILIMANJARO” ,ALTEZZA WATOA VIFAA VYA MIL 210

Image
Kontena maalumu lililowekwa vifaa kwa ajili ya zoezi la uzimaji moto endapo utatokea katika Hiafadhi ya Taifa ya Kilimanjaro . Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry Andreichuk  (kushoto) akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) wakati akikabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto . Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry  Andreichuk  (kushoto) akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) wakati akikabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto  Mkurugenzi wa Kampuni ya Altezza Travel ya mjini Moshi  Dmitry  Andreichuk  akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa kontena sita lililosheheni vifaa vya kuzimia moto kwa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro. Baadhi ya vifaa maalumu kwa ajili ya kuzima moto katika maeneo yeny miinuko vikiwa katika kontena zilizo

MWISHAWA NAIBU KAMISHNA MPYA TANAPA

Image
ARUSHA  Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Mussa Nassoro Kuji ameongoza uapisho wa Naibu Kamishna mpya wa Uhifadhi Massana Gibril Mwishawa anayeshughulikia Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara katika Shirika la Hifadhi za Tanzania (TANAPA). Hafla ya uapisho iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA   jijini, Arusha imeambatana na uvishwaji wa cheo kipya cha Naibu Kamishna wa Uhifadhi   ambapo katika salamu za Pongezi Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Musa Kuji amesisitiza uwajibikaji na kumtanguliza Mungu katika kutekeleza majukumu hayo ya Naibu Kamishna wa Uhifadhi.   ”Cheo huambatana na majukumu na uwajibikaji. Hivyo basi, ni muhimu ukamtanguliza Mwenyezi Mungu wakati wote ili aweze kukuongoza katika utekelezaji wa majukumu yako haya mapya. Taaluma, uzoefu, umahiri na kujituma kwako, kunatupatia imani kubwa kuwa utatekeleza majukumu yako kwa uadilifu, weledi, bidii kubwa na bila woga wala upendeleo” alisisitiza Kamishna Kuji   Aidha, Kamishna Kuji aliongeza kuwa katika nafasi ya Naibu Kamishna wa

"ARUSHA NI TAJIRI TUKIYAELEWA MAONO YA RAIS SAMIA"- RC MAKONDA

Image
Arusha  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda usiku wa Ijumaa Juni 08, 2024 amewasihi Waongoza watalii wa Mkoa wa Arusha kuwa waadilifu, wenye lugha nzuri na vinara wa kuutangaza vyema Ukarimu wa Watanzania kwa kila Mgeni na Mtalii watakaebahatika kumuhudumia ndani ya Mkoa wa Arusha. Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa msimu wa tisa wa programu ya "Safari Field Challenge" yenye lengo la kumpata Mwongoza watalii bora wa mwaka, Shughuli iliyofanyika kwenye ukumbi wa Grand Melia Jijini Arusha ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas aliyemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki. Katika hotuba yake Mhe. Paul Makonda amewapongeza waongoza watalii hao kwa kazi nzuri akiwasisitiza kuwa wao ndiyo mabalozi wakuu wa kudhihirisha kwa vitendo kauli za Rais Samia Suluhu Hassan alizozitoa wakati wa filamu ya The Royal Tour pamoja na mahojiano mbalimbali kwenye vyombo vya habari vya

RC MAKONDA AAGIZA POLISI KUTOSIMAMISHA MAGARI YA UTALII BARABARANI

Image
  Ataka Teksi zote kuwa na rangi ya kufanana  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kutokukamata magari ya Utalii kwenye Mkoa wa Arusha na badala yake ukaguzi kwa watalii ufanyike kwenye mipaka na kwenye viwanja vya ndege vinavyotumika na watalii. Mhe.Makonda amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo Juni 08, 2024 kwenye Viwanja vya Magereza Kisongo, Ikiwa ni siku ya ya maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu Kili Fair 2024, yakijumuisha makampuni zaidi ya 700 ya kimataifa kutoka kwenye mataifa zaidi ya 50. Katika hatua nyingine pia Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Arusha ametoa miezi miwili kwa magari (Teksi) zinazotumika kubeba wageni na watalii wa Mkoa wa Arusha kuwa na rangi maalumu za kufanana ili kutoa  urahisi kwa mtalii kulifahamu gari husika pamoja na kutoa hakikisho la usalama kwa wageni na watalii wanapoamua kutumia aina hiyo ya usafiri wawapo Jijini Arusha. Mhe. Makonda amechukua hatua hiyo ili kuendelea kuunga

WANAFUNZI KUTOKA CHUO CHA UTALII PASIANSI WAPATA ELIMU YA USALAMA WA WATALII.

Image
Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi. Wanafunzi toka Chuo cha Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi kutoka Mkoani Mwanza leo wamefika Katika kituo cha Polisi cha Utalii na Diplomasia Jijini Arusha kwa ajili ya kujifunza namna ambavyo Kituo hicho  kinafanya  kazi ya kuwahudumia Watalii na Wageni wanaofika Mkoani humo.  Mkuu wa Kituo hicho, Mrakibu wa Polisi SP Waziri Tenga amebainisha kuwa wanafunzi hao wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuzingatia usalama wa watalii na wageni pindi wanapowahudumia. Sambamba na hilo SP Tenga amewasihi Wanafunzi hao kuhakikisha wanakwenda kutoa huduma bora kwa watalii kwa sababu wageni wengi huwa wanatarajia kuona wanapata huduma bora pindi wanapofika Nchini. Aidha SP Tenga amewaeleza namna ambavyo kituo hicho kimeimarisha mahusiano mazuri kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Sheria, taasisi za Kimataifa lakini pia makampuni yote ya utalii lengo likiwa ni kufikia lengo la Serikali la kuhakikisha watalii na wa