Posts

MKURUGENZI MOSHI ATOKWA MACHOZI ,CCM NA CHADEMA WAKIMPA ZAWADI .

Image
Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri . Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo akizungumza jambo katika kikao hicho ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe . Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi wakikabidhi keki kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe kama zawadi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akipokea zawadi ya seti ya vyombo kwa ajili ya chakula kutoka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri. Diwani wa kata ya Kiboriloni Frank Kagoma (Chadema)  akiwaamebeba zawadi ya j...

MAPATO MANISPAA YA MOSHI "YAPAA" KUTOKA BILIONI 6.1 HADI BILIONI 9.9

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo akitangaza ongezeko la mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi . Mkurugenzi wa Hlamshauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akizungumza wakati wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi . Baadhi ya Wakuu wa Divisheni na watendaji katika ofisi za Halmashauri ya Manipaa ya Moshi wakifuatilia kikao cha Bajeti cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo. Baadhi ya Madiwa wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakichangia mjdala wa Bajeti ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakati wa kikao cha Bajeti .  Na Dixon Hussein - Moshi   Manispaa ya Moshi imepiga hatua kubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani, ikiongeza mapato kutoka bilioni 6.1 mwaka 2021 hadi bilioni 9.9 mwaka 2025, ongezeko la takribani bilioni 3.7. Mafanikio haya yanatajwa kuwa matokeo ya mikakati madhubuti iliyowekwa ili kuboresha vyanzo vya mapato na kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma. Akizungumza katika kikao cha bajeti...

BILIONI 4 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KONDOA ,DC NYANGASA AONYA

Image
  Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa Bi Dollah Kilo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi na vyanzo vya maji katika wilaya hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akiwa ameongozana na watendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira pamoja na Ruwasa Kondoa alipotembelea ofisi mpya za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa . Sehemu ya miundombinu ya maji kwa ajii ya ukamilishaji wa mradi mkubwa wa Maji wa Bilioni nne uliotolewa na Serikali kwa ajili ya kunguza changamoto ya Maji kwa wananchi wa wilaya ay Kondoa . Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akioneshwa jambo na Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kondoa Mhandisi Merinyo wakati wa ziara yake ya kutembelea vyanzo vya maji . Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Fatma Nyangasa akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kondoa Bi Dollah Kilo wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi n...

BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI

Image
 BILIONI 100 ZATUMIKA KUSAMBAZA UMEME KIGOMA VIJIJINI #KAZIINAONGEA  Katika kuendelea  kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.   Katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kwa sasa serikali inapeleka umeme kwenye vitongoji ambapo Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi. Aidha Katika vitongoji 1849 vya  Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme.

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA

Image
 SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ZIWA VICTORIA #KAZIINAONGEA Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa Maji kwa  wananchi wake, hivyo inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo ni Mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia vijiji 9 na Mradi wa Nkinga Simbo utakaohudumia vijiji 8 vilivyopo jimbo la Manonga Mkoani Tabora. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Manonga Seif Gulamali, aliyeuliza lini Serikali itatenga Fedha za ujenzi wa Miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale - Manonga. Mhandisi Kundo amesema Mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata za Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilisha miradi hiyo. Amesema  Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa vijiji vya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika kata...

SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000

Image
 SERIKALI YATAKA GHARAMA YA UMEME KWA VIJIJI VYOTE IWE 27,000 #KAZI INAONGEA Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetaka gharama ya kuweka umeme kwa vijiji vyote nchini iwe ji tsh.27,000 na sio zaidi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Jijini Dodoma hivi karibuni. Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, Kapinga alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,  Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili yaweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000. Akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme ya  zaidi ya 27,000. "Kuna baadhi ya maeneo ambayo ni Vijiji yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, , namuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kufanya mapitio ya ma...

MFANYABIASHARA MOSHI AGAWA MITAJI YA MIL 10 KWA MARAFIKI ZAKE .

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa bidha mbalimbali kwa kundi la Wafanyabiashara wadogowadogo walioanza Biashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya ZAC Enterprisesya mjini Moshi . Baadhi  ya Wafanyabiashara wadogowadogo katika kundi la Wamachinga 50 walionufaika na msaada kwa ajili ya kukuza mitaji kutoka kampuni ya ZAC Enterprises ya mjini Moshi  Mkurugenzi wa Kampuni ya ZAC Enterprises Izack Ngowi akioa maelezo kuhusu baadhi ya bidhaa alizokabidhi kama msaada kwa ajili ya kukuza mitaji kwa Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Wamachinga alioanza nao biashara. Baadhi ya Wafanyabiashara wakipokea sehemu ya bidhaa zilizotolewa kwao na Kampuni ya ZAC Enterprises kwa ajili ya kukuza mitaji yao  Sehemu ya msaada uliotolewa kwa Wafanyabiashara marafiki wa Izack Ngowi ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya ZAC Enterprises kwa ajili ya kukuza mitaji yao. Baadhi ya wafanyabiashara walionufaika na mtaji kutoka kwa Kampuni ya ZAC Enterpr...