Posts

Showing posts from February, 2014

Tizama.MAELFU WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA KILIMANJARO MARATHONI 2014.

Image
Katika banda la Vodacom shughuli za uandikishaji kwa wakimbiaji wa mbio za Km 5 Fun Run zikienndelea. Kampuni ya GAPCO pia wapo kuhakikisha mbio za walemavu zinafana mwaka huu Kwa wale wanaokimbia wakitizama muda hawa jamaa pia wamepiga kambi Keys Hotel. Upande wa wadhamini wakuu mbio hizo Kilimanjaro Premium Lager shughuli za uandikishaji ziliendelea. Shirika linalopambana na masuala ya Ukeketaji NAFGEM pia wanahkikisha watoto wa jamii ya kimaasai wanashiriki mbio hizo. Mazingira ya mji wa Moshi tayari yamebadilika ikiwa ni shamrashamra ya mbio hizo.

NYAMA CHOMA KUKOSEKANA KILIMANJARO MARATHONI NI BAADA YA WAUZAJI KUGOMA KUCHINJA.

Image
Wauzaji wa Nyama wakiwa nje ya mabucha yao baada ya kugoma kuuza nyama. Baadhi ya mabucha yaliyofungwa. Moshi WAKAZI wa mji Manispaa ya Moshi, wametaabika kwa siku mbili sasa wakiwa hawapati kitoweo cha Nyama baada ya halmashauri ya manispaa hiyo na mamlaka ya udhibiti wa Chakula na dawa TFDA kuyafunga maduka ya nyama ambayo hayakidhi vigezo vya afya. Katika hali inayoonesha kuwapo kwa mgomo wa wauza nyama,pamoja na manispaa kuyafunga maduka sita ambayo yalibainika kutokidhi vigezo,lakini manispaa hiyo yenye maduka zaidi ya 50, lakini hakuna hata moja linaloendelea na biashara hiyo. Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wenzake, Damian Temba alisema pamoja na kwamba manispaa ilitoa muda wa wafanyabiashara kuyafanyia marekebisho maduka yao lakini bado masharti waliyoweka hayatekelezeki. "Tulipewa notisi yenye masharti 16, ikiwamo bucha kuwa na kiyoyozi, msumeno maalum wa kukata nyama,kuwapo kwa vioo na leseni ya TFDA.......hii misumeno haipatikani

EXTRA BONGO KUPAGAWISHA MKESHA KILI MARATHONI.

Image
George Kavishe Moshi. WASANII mbalimbali wanatarajia kutoa burudani kesho usiku katika Ukumbi wa Voda House mjini Moshi ikiwa ni mkesha kabla ya kufanyika kwa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon Jumapili zitakazoanzia katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika. Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema jijini Dar es Salaam jana kuwaburudani hiyo ni moja ya hamasa kabla ya kufanyika kwa mbio hizo. Aliwataja wasani watakaotoa burudani katika siku ya mkesha huo wa Kilimanjaro Marathon kuwa ni Jambo Squad, Jambo squad  The Warriors.   The warrios Extra Bongo. Xtra Bongo   Joh Makini “Kwa mwaka huu tumeona tufanye tofauti kwa kuweka burudani katika siku ya mkesha kabla ya kufanyika Kilimanjaro Marathon,” alisema. Alisema pia siku ya mashindano hayo ya Kilimanjaro Marathon kutakuwepo na burudani kutoka kwa Joh Makini, Jambo Squad, Wakali Dancers na FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma. Mbio hizi zinaratibiwa

NJIA YA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON ZAPIMWA NA KURIDHIWA

Image
NJIA mpya zitakazotumika wakati wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro mwaka huu, (Kilimanjaro Marathon 2014), zimepimwa na kuridhiwa ambapo mabadiliko hayo yameboreshwa ikilinganishwa na njia za zamani.  Kwa mujibu wa waandaji, marekebisho hayo yamelenga kuboresha usalama barabarani na kuondoa msongamano wa magari wakati yanaendelea. Njia zilipimwa na kuridhiwa na katibu wa chama cha kimataifa cha mbio ndefu, (AIMS), Hugh Jones akisaidiana na Michael Hughes wa Nairobi Marathon, Ibrahim Hussein wa shirikisho la vyama vya riadha vya kimataifa, (IAAF), pamoja na John Bayo wa Kilimanjaro Marathon Club.   Akitoa maoni yake kuhusu njia hizo mpya Jones, alisema “Njia hizi mpya ni nzuri na za kuvutia. Hapa utaona kuwa baada ya kuanza kwa nusu marathon na kuingia nusu ya pili ya mbio hizi kwa ujumla, washiriki watajikuta wakijitahidi kupanda kilima.  Hii ni sehemu ngumu yenye kuchosha lakini washiriki watakutana na mashabiki wengi watakaokuwa wakiwashangilia na kuwatia moyo. Waki

MSHITAKIWA KESI YA KUSAFIRISHA TWIGA AUGUA GHAFLA

Image
Moshi MAHAKAMA ya hakimu mkazi mjini Moshi jana imelazimika kuahirisha kesi ya utoroshwaji wa Twiga kwenda Uarabuni baada ya mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo Kamran Ahmed,kuugua ghafla muda mchache kabla ya kufika mahakamani hapo. Kwa mujibu wa wakili wa mshtakiwa huyo Edmund Ngemela aliieleza mahakama hiyo kwamba mshtakiwa huyo Sukari imepanda na hivyo kushindwa kufika mahakamani kuendelea na kesi inayomkabili. Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Simoni Kobelo na mawakili wa pande zote mbili, Ngemela alisema kulingana na hali ya afya ya mteja wake ilikuwa ni vigumu kufika mahakamani hapo. "Mheshimiwa hakimu kesi hii ilikuja kwa ajili ya kuendelea na mashahidi upande wa mashtaka,lakini niiombe mahakama yako tukufu, kuaihirisha kwani mteja wangu, sukari imepanda kuliko kiwango cha kawaida"alisema Katika kesi hiyo iliyolazimika kuzungumzwa katika mahakama ya ndani(Chamber court) upande wa mawakili wa serikali haukuwa na pingamizi na maombi hayo na kutaka mahakam

MAANDALIZI KILIMANJARO MARATHONI HAYA HAPA.

Image
Mabango mbalimbali ya wadhamini wa mbio za Kimatafa za Kilimanjaro marathoni tayari yameanza kuupamba mji wa Moshi. Mkurugenzi wa mbio za Kilimanjaro marathoni 2014, John Bayo akizungumzia njia mpya ambazo wakimbiaji watazitumia mwaka huu. Ramani ya njia itakayotumika kwa wakimbiaji wa mbio za kujifurahisha za Vodacom fun run. Ramani ya njia itakayotumika kwa wakimbiaji wa mbio za Full marathon,half marathoni pamoja na mbio za walemavu.

2014 KILIMANJARO MARATHON STADIUM ACCESS AND SECURITY ADVISORY

Image
1.  The roads from Arusha Roundabout to approximately 10 kilometres out on Taifa Road will be closed from 6:15am to 8:00am. 2.   Sokoine road from MUCCoBS to KCMC - Kibosho Corner, and from Lema Road to MUCCoBS  through Kilimanjaro Road will be closed from 6.30am to 8.00am. 3. There will be traffic control and restricted access from YMCA – CLOCK TOWER – BOMA RD – ARUSHA ROUNDABOUT – URU RD – MUCCOBS from 7.30am to 8.15am. 4. Note – drivers using these roads after they have been opened to traffic are asked to drive with caution and look out for slower runners who will still be on the route. 5. It us suggested that tour operators collecting climbers from Mweka should do so after 9.00am and use Mweka / Sokoine Rd , as this will be clear of runners by then. 6. Motorists are advised to avoid Lema Rd / Kilimanjaro Road / Muccobs Main Gate roads if at all possible. 7. Buses are advised not to leave Moshi for Dar before 8:00am. You can leave Moshi for Arusha via A